Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. 9PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. Kutoka kulia ni Rais wa taasisi hiyo, Ali Akkiz na Mshauri wa masuala ya Habari, Felix Kaiza.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mshauri wa Masula ya Habari, Felix Kaiza akielezea umuhimu wa wamiliki wa vyombo vya habari kuweka utaratibu wa mafunzo ya ndani (In House Training) kwa waandishi wa habari ili kuinua weledi pia alishauri kuwepo na Exchange Program kati ya vyombo vya habari nchini na nje ya nchini jambo ambalo huwaongezea uwezo wanahabari.
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, Esther Zaramula akielezea kwenye mjadala huo jinsi alivyonufaika na mpango wa kubadilishana uzoefu
Habib Miradji akisisitiza jambo wakati wa mjadala huo ambapo alifafanua zaidi umuhimu wa wanahabari kuandika habari kwa kufuata maadili na kusimamia kwenye ukweli.
Pia katika kongamano hilo waliwaasa wanahabari kutojiingiza katika mkumbo wa kuingizwa mifukoni mwa wanasiasa na matajiri kwa kuandika habari za kuwasifia wao badala ya maslahi ya wananchi.
Mwandishi wa habari, Ezekiel Kamwaga akielezea umuhimu wa wanahabari kujiendeleza kielimu pamoja na vyombo vya habari kubadilika kwa kwendana na kasi ya mabadiliko ya kizazi hiki cha maendeleo ya teknolojia ya habari.
Rais wa taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Ali Akkiz aktoa shukrani kwa wanahabari walioshiriki kwenye mjadala huo uliofanikiwa.
No comments:
Post a Comment