Charles Ekelege |
Na Mwene Said wa Blogu ya
Jamii
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekelege amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miaka mitatu na kuilipa serikali Dola 42,543 za Kimarekani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS), Charles Ekelege amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwenda jela miaka mitatu na kuilipa serikali Dola 42,543 za Kimarekani, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50.
Kadhalika, Ekelege
anadaiwa kutoa asilimi hiyo ya punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni
mbili Kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage na Kampuni Quality Motors na
kulisababishia shirika hilo hasara ya dola hizo.
Hukumu hiyo imetolewa leo
na Hakimu Mkazi Augustina Mmbando baada ya kupitia ushahidi wa pande zote
mbili na mahakama yake kumuona mshtakiwa bila kuacha shaka ana hatia.
Hakimu alisema ushahidi
uliotolewa na upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kwamba mshtakiwa kupitia
wadhifa wake alifanya maamuzi bila kinyume na sheria za TBS zinazomwelekeza
kuwasilisha masuala yote ya kiutendaji kwenye Bodi ya Wakurugenzi.
Alisema kitendo cha kutoa
msamaha kwa kampuni hizo bila kuacha shaka moja kwa moja mahakama imeona
alitumia madaraka yake vibaya.
“Kwa upande wa
shitaka la pili, kiongozi yeyote katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania anapokuwa madarakani ni kwa ajili ya maslahi ya taifa, lakini
mshtakiwa alikosa uzalendo na kutumia madaraka yake vibaya kuhujumu uchumi”
alifafanua hakimu kuhusu ushahidi wa Jamhuri.
“Mahakama inamuona
mshtakiwa ana hatia katika kosa hili la pili la kujumu uchumi … pia mshtakiwa
amesababisha watanzania waliompa dhamana kukosa kula keki ya taifa lao kwa
kujinufaisha yeye binafsi” alisema hakimu huyo na kuongeza kuwa.
“Katika ushahidi
uliotolewa na mshtakiwa alikiri kufanya maamuzi bila kupata baraka na kibali
cha Bodi ya Wakurugenzi na kwamba aliidanyanya mahakama” alisema Hakimu
Mmbando.
Akifafanua zaidi alisema
mshtakiwa alidai kuwa katika kutoa maamuzi pinguzo kwa kampuni hizo
alishirikisha menejimenti na kwamba shirika lilikuwa na utaratibu wa kufanya
kikao kila siku asubuhi.
Hata hivyo, shahidi wa
pili wa utetezi Thomas Mlugulu alishindwa kuieleza mahakama wajumbe waliokuwa
wakihudhuria kikao cha cha asubuhi cha shirika kwa kila siku zaidi ya kumtaja
Betwel Matemba ambaye alishakufa na hawezi kufika mahakamani.
Alisema ushahidi wa
utetezi ulikuwa dhaifu kushindwa kukanusha ushahidi wa Jamhuri ulioweza kuithibitishia
mahakama ukweli kuhusu mashitaka yanayomkabili Ekerege.
Hakimu alisema mahakama
pia inamtia hatia mshtakiwa kwa shitaka la tatu la kuisababishia serikali
hasara ya dola hizo na kuwasababishia watanzania kukosa kula keki ya taifa lao.
Hakimu Mmbando alitoa
nafasi kwa mawakili wa pande zote mbili kutoa hoja kabla ya kusoma adhabu.
Mwendesha Mashitaka wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Janeth Machulya, alidai
kuwa kulingana na makosa aliyotiwa hatiani mshtakiwa kwamba alipewa dhamana na
rais pamoja na watanzania lakini aameshindwa kuwa mzalendo.
“Kwa kuwa mshtakiwa
ameshindwa kuwa mzalendo kwa mamlaka aliyopewa na wananchi, tunaomba mahakama
itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa vigogo wote wanaopewa madakara na
kuyatumia vibaya,” alidai na kuongeza.
“Mheshimiwa kwa kosa la
uhujumu uchumi mahakama izingatiee utoaji wa adhabu kulingana na sheria ya kosa
hilo inavyoelekeza” alisema Machulya aliyeongoza mashahidi wa Jamhuri katika
kesi hiyo na mahakama kumtia hatiani kigogo huyo.
Wakili wa utetezi Majura
Magafu alidai kuwa mahakama imuonee huruma mshtakiwa kwa sababu ana familia
inamtegemea.
Pia, wakili huyo alidai
kuwa mshtakiwa anajutia makosa aliyofanya na kwamba akipewa nafasi hawezi
kurudia.
Hukumu hiyo iliyoanza
kusomwa saa 6:20 mchana hadi saa 8:10 hakimu aliahirisha kwa nusu saa kabla ya
kusoma adhabu.
Saa 8:49 mahakama
iliyoketi chini Hakimu Mmbando ilianza shughuli zake.
Akisoma adhabu hiyo,
hakimu alisema Viongozi wote wa serikali wako juu kwa ajili ya kulinda maslahi
ya taifa ili kulinda na kuangalia nchi na mali zake, siyo kuongoza kwa matakwa
ya kiongozi husika.
“Mshtakiwa unastahili
kuhukumiwa ili kuwa mfano kwa viongozi wengine wanaochezea keki ya taifa hili
kwa manufaa yao binafsi… unakwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kwanza, mwaka
mmoja kwa kosa la pili na mmoja mwingine kwa kosa la tatu na ailipe serikali
fedha alizoisababisha hasara” alisema Hakimu Mmbando.
Baada ya hukumu kusomwa;
Mshtakiwa alianza
kububujikwa na machozi huku watu wanaodaiwa kuwa familia yake wakiangua vilio
kwa sauti wakati mpendwa wao akiwa chini ya ulinzi tayari kwenda gerezani
kuanza kutumikia kifungo.
Watu mbalimbali waliokuwa
katika viunga vya mahakama hiyo walimzunguka mshtakiwa huyo huku kila mmoja
akisema lwake’jamani jela ni jela’ wengine ‘tatizo hizo fedha alizoambiwa alipe
anazo au alishakula zote’ walisikika wakizunguma.
Mapema Mwaka 2012, aliyekuwa
Waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami aliondolewa katika wadhifa huo
kutokana na kashfa ya kutoa punguzo la tozo na baadaye Mei 21, mwaka 2012,
mshtakiwa alisimamishwa kazi kama Mkurugenzi wa TBS ili kupisha uchunguzi na
hatimaye jana kuhumiwa.
Katika kesi ya msingi,
Ekelege anadaiwa kuwa kufanya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50
ya punguzo la tozo ya utawala kwa kampuni hizo mbili.
Pia, ilidaiwa kuwa Machi
28, mwaka 2008 na Agosti 7, mwaka 2009, katika ofisi za TBS zilizopo wilaya ya
Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwa nia ovu Ekerege alitumia madaraka yake
vibaya.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa
huyo alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa punguzo la asilimia 50 ya ada ya
utawala kwa kampuni hizo bila idhini ya baraza la utendaji la TBS kinyume cha
sheria namba 2 kifungu kidogo cha (3) ya TBS ya mwaka 2005.
Ilidaiwa kuwa kitendo
hicho kiliziongezea kampuni hizo faida ya Dola 42,543 za Kimarekani sawa na
(kwa wakati huo) Sh. Milioni 68,068,800.
Upande huo wa Jamhuri
ulidaiwa shitaka la pili, katika tarehe na mahali pa tukio la kwanza, mshtakiwa
alilisababishia shirika kupata hasara ya fedha hizo.
No comments:
Post a Comment