Tangazo

August 28, 2014

BIOLANDS YAKABIDHI MSAADA WA AMBULANCE NISSAN PATROL KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA


Gari la Kubebea wagonjwa likiwa linaingia kwa ajili ya Makabidhiano
Meza kuu


 Meneja Mkuu msaidizi wa Biolands(Kulia) akimkabidhi na kupongezana  na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga ufunguo wa Gari la Wagonjwa katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Halmashauri ya Wilaya Kyela.
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Malenga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Gari la Wagonjwa walilokabidhiwa na kampuni ya Biolands , akisaidiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Seif Mhina 
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga  akifungua Mlango wa Gari la Wagonjwa Kuashiria Uzinduzi 
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akiwasha Gari la wagonjwa 
 Meneja wa Biolands Tawi la Kyela Erasto Kilongo akisoma  Risala kwa Mgeni Rasmi kabla ya Makabidhiano ya Gari ya wagonjwa 
 Mwenyekiti wa Bodi ya uhamasishaji wa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (HIMSO) Dkt. Charles Mbwanji akitoa salamu za shirika lake katika sherehe za makabidhiano ya Gari 
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Seif Mhina akizungumza wakati wa Sherehe za Makabidhiano ya Gari la wagonjwa
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Clemence Kasongo akitoa Shukurani kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri Baada ya kukabidhiwa msaada wa Gari 
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akitoa Hotuba yake kwa wageni waalikwa na wananchi wa Wilaya ya Kyela Baada ya Kukabidhiwa msaada wa Gari ya Wagonjwa na Biolands
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Gabriel Kipija akitoa shukurani za Halmashauri kwa kampuni ya Bioland baada ya kukabidhiwa Msaada wa Gari la Wagonjwa.
 Meneja Mkuu Msaidizi wa Biolands Felix Mtawa akitoa neno la utangulizi kabla ya Kukabidhi Msaada wa Gari ya Wagonjwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela


Wananchi na Wageni mbalimbali waliohudhuria Sherehe za makabidhiano ya Gari la wagonjwa wakifuatilia kwa makini tukio hilo

*****************


KAMPUNI ya Biolands International Ltd imetoa msaada wa gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) aina ya Nissan Patrol kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela lenye thamani ya shilingi zaidi ya Milion 76.

Hafla ya makabidhiano ya gari hilo imefanyika  katika viwanja vya Halmashauri hiyo baina ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Esther Malenga, Meneja wa Bioland Felix Mtawa na Mwenyekiti wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya, Dk.Charles Mbwaji wakishuhudiwa na mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina.

Katika Risala ya Bioland iliyosomwa na Meneja wa Tawi, Erasto Kilongo, alisema lengo la msaada huo ni kutambua mchango wa wananchi katika maeneo wanayofanya kazi.

Alisema Bioland ni Kampuni Binafsi inayojishughulisha na ununuzi wa Kakao katika Wilaya za Kyela na Rungwe ambapo   inafanya kazi na na wakulima zaidi ya 20,000 katika vituo 137 vilivyopo katika wilaya hizo mbili.

Alisema Kampuni hiyo inafanya kazi moja kwa moja na wakulima katika kufanikisha shughuli za vyeti mbalimbali ambavyo vinasaidia kuwepo kwa uhakika wa soko la kakao, vyeti kama vile kilimo hai (organic farming), Kilimo endelevu (Rain forest Allience),na  Usawa wa kibiashara katika jamii (social and Fare Trade).

Alisema katika sekta ya Afya na usalama wa wazalishaji, Kampuni  imenuia kuhakikisha afya za wakulima na familia zao zinaendelea kuimarika wakati wote na kupata huduma za afya kwa gharama nafuu kupitia mradi wa Bima ya afya ya jamii.

Alisema  katika kufanikisha mradi huo, Kampuni  ilikubali kutenga kiasi cha dolla 60,000 za kimarekani kwa kipindi cha miaka 5 toka 2010 hadi 2014 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa wakulima wanaojiunga na bima ya afya ya jamii.

Aliongeza kuwa  Kutokana na umuhimu huu wa kuhakikasha afya za wakulima na familia zao zinaimarika pia Biolands imefadhili ununuzi wa gari la wagonjwa (Ambulance)  lenye thamani  Shilingi Milioni 76,140,000/=, ambalo  limekabidhiwa kwa Halmashauri kwa niaba ya CHIF, HIMSO, CIDR na wananchi wa Kyela.

Awali akitoa salamu kwa niaba ya HIMSO, Dk. Charles Mwanji, alisema kazi ya HIMSO ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali ni kuhakikisha wananchi wanajiunga na mfuko wa jamii na kupata huduma ipasavyo.

Alisema moja ya majukumu yao ilikuwa ni kuwahamasisha Bioland kununua gari la wagonjwa kutokana na umuhimu kwa Wananchi wa Kyela ili waweze kupata huduma za mfuko wa bima kiufasaha.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina, alisema Kazi ya Bioland na HIMSO ilikuwa ni kutoa gari hivyo Halmashauri ihakikishe gari linatumika katika shughuli iliyokusudiwa.

Alisema ili hayo yakamilike ni bora gari hilo likawa linashindwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kyela ili kuepuka matumizi tofauti ya gari kama ilivyowahi kutokea kwa magari mengine.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela ikishukuru kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kyela, alisema Kampuni hiyo imemaliza kilio cha Wananchi wa Kyela cha kutaka gari la wagonjwa kilichokuwepo muda mrefu.

Alisema kupitia hamasa walioonesha Bioland Wilaya yake itaanza kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili kuhakikisha kila mwananchi anatumia kadi kwenye matibabu.

Aidha alitoa wito kwa watumishi wa vituo vya Afya na Mahospitali kutoa kipaumbele kwa wagonjwa wenye kadi kuliko wenye fedha mkononi ili wapate tiba kama serikali ilivyoagiza.

No comments: