Ofisa mauzo wa Isere Sports, Rasul Nkusa akionesha aina ya mpira na raba mpya zilizowasili nchini. |
Hizi ni baadhi ya truck Suits zilizowasili Isere Sports. |
Meneja Masoko wa Isere
Sports, Abas Isere akionesha skafu na kofia za bendera ya taifa zilizowasili
nchini.
|
Hizi ni baadhi ya jezi
zilizowasili kwa ajili ya kuusambaza kwa wadau wa michezo Tanzania na nje ya
nchi kulia ni Ofisa Masoko Msaidizi, Ismail Bura.
Na
Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya
Isere Sports inayoagiza na kuuza vifaa vya michezo nchini imepokea shehena
kubwa ya mali mpya ya vifaa vya michezo kutoka Dubai na China.
Mkurugenzi
wa Michezo wa Isere Sports, Abas Isere alisema jana kuwa vifaa hivyo vyenye ubora
unaokubalika vimewasili na tayari vimeanza kusambazwa kwenye ofisi zao zilizopo
mtaa wa Mchikichi na Living Stone, Karikaoo na jingine la Dodoma.
Alisema vifaa vilivyowasili ni truck
suits za rangi mbalimbali, jezi za mpira wa miguu, netiboli, wavu, basketi
ambavyo vyote vinauzwa kwa bei nafuu na kutoa wito kwa maofisa kutoka taasisi
mbalimbali za Serikali kutoa oda zao mapema.
Vifaa vingine vilivyowasili ni matufe,
mikuki, visahani, vikombe, mipira ya michezo yote, raba za michezo, viatu vya
mpira na vingine vingi ambavyo vinafaa kutumika kwenye mashindano mbalimbali
nchini.
Kwa mawasiliano
zahusiana na vifaa vya michezo mbalimbali wasiliana na 0713241470
No comments:
Post a Comment