Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea soko la nafaka la
kimataifa la Kibaigwa mkoani Dodoma katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani
humo Agosti 28, 2014, ambapo alijionea shehena kubwa sana ya mahindi iliyoletwa
kutoka mashambani na kusafirishwa kila pembe ya nchi. Mwaka huu, kama
ilivyokuwa mwaka jana, mavuno ya mahindi yamekuwa makubwa kiasi hata cha
kupatikana kwa mavuno ya ziada yanayolemea maghala yaliyopo, ikiwa ni
muendelezo wa mafanikio ya sera ya kilimo kwanza ambayo imekuwa ikileta matokeo
mazuri kila mwaka. PICHA NA IKULU
|
No comments:
Post a Comment