Tangazo

August 30, 2014

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH. JANETH MBENE ATEMBELEA BANDA LA NSSF MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI KANDA YA KATI

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeshiriki kwenye maonesho ya wajasiriamali Kanda ya Kati yanayofanyika Mkoani Kigoma kwenye viwanja vya Community Centre kuanzia Tarehe 27/08/2014 mpaka tarehe 02/09/2014.

Katika Maonesho hayo NSSF imekuwa ikitoa Elimu ya Uanachama wa HIARI kwa Wajasiriamali wanaoshiriki kwenye maonesho hayo na kuandikisha wanachama kwa HIARI. Pia NSSF inatoa Elimu kwa wajasiliamali jinsi ya kukopa NSSF kupitia SACCOS.

Mgeni Rasmi, Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene aliwapongeza NSSF kwa kushiriki kwenye maonesho hayo na pia kwa juhudi zao za kutoa elimu kwenye maonesho mengi .
Mgeni Rasmi aliusifia mpango wa Wakulima Scheme kwa kuweza kuwafikiria wakulima na kuwapa mafao ya hifadhi ya jamii.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Kigoma, Josephat Komba akimuelezea Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF kwenye banda lao wakati wa maonesho ya wajasiriamali Kanda ya Kati.
 Banda la NSSF linavyooneka kwenye maonesho ya Wajasiriamali wa Kanda ya Kati yanayofanyika 
 Maofisa wa NSSF walioshiriki Kwenye Maonesho ya wajasiriamali kanda ya Kati wakiwa na Meneja wa Mkoa wa Kigoma, Josephat Komba wakimsubiri Mgeni Rasmi kuja kutembelea banda la NSSF.
Daktari wa NSSF akimpima Shinikizo la Damu Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF ,Theopista Muheta wakati wa maonesho ya wajasiriamali anda ya kati.
Mmoja ya Washiriki wa Maonesho ya Wajasiliamali Kanda ya kati akipima uzito tayari kupewa Ushauri juu ya uwiano wa uzito wake na urefu (BMI) na Daktari wa NSSF.
 Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wakipata maelekezo ya Mafao yatolewayo na NSSF kwa wanachama wa Hiari na wasio wa Hiari.

No comments: