Chalinze, Pwani
Mtu mmoja ambaye hakujulikana jina, amekutwa akiwa amejinyonga
ndani ya kibanda shambani huku akiwa na karatasi iliyoandikwa ujumbe “Nawaachia
dunia yenu muishi miaka 110”.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibiki, Ally Hussein alisema kijana
huyo mwanamume amekutwa saa mbili usiku akiwa amefariki na hivyo kutoa taarifa
katika Kituo cha Polisi Chalinze.
Alisema askari walifika na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa
umefungwa kamba ya katani na alipopekuliwa alikutwa mfukoni na karatasi yenye
maandishi hayo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Mrakibu Msaidizi, Athumani
Mwambalaswa amethibitisha tukio hilo na kusema mwili wa marehemu ulichukuliwa
na kuifadhiwa Kituo cha Afya Chalinze kusubiri uchunguzi wa daktari.
Hata hivyo, alisema bado haijafahamika mtu huyo ni mwenyeji wa
kijiji kipi kwani hapo Kibiki hakuweza kutambulika na jitihada za kutafuta
ndugu zake katika vijiji vya jirani zinafanyika. Chanzo cha kujinyonga bado
hakijajulikana.
No comments:
Post a Comment