Tangazo

September 12, 2014

Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari Dar

Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 4.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mwakilishi wa Afisa Elimu ya Sekondari Manispaa ya Temeke, Yasintha Kayoza kwa niaba ya shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario.  
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (mwenye miwani), akiangalia moja ya vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 4.5/-, baada ya kuvikabidhi kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mbagala jijini Dar es Salaam jana. 
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 1.5/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbagala, Mwalimu Marcelina Kimario katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana. Sekondari nyingine zilizokabidhiwa vitabu hivyo ni pamoja na Mvuti na Kambangwa. Kushoto ni Mwakilishi wa Shule ya Sekondari Kambangwa, Mwalimu Sueiba Mfinanga.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbagala wakifurahia vitabu vya masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa  ‘Shule Yetu’ kukabidhi vitabu hivyo vyenye thamani ya milioni 4.5/- kwa shule tatu za sekondari za Mbagala, Mvuti na Kambangwa katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Zaidi ya shule 30 kufaidika na msaada wa vitabu kwa mwaka huu,  kupitia mradi wa Airtel “Shule yetu”

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa “shule yetu” umeendelea na mpango wake wa kuchangia katika kusaidia sekta ya elimu nchini ambapo  jana imetoa msaada wa vitabu kwa shule 3 za sekondari jijini Dar es saalam.

Shule zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na Kambagwa sekondari iliyopo wilaya Kinondoni,  shule ya sekondari Mvuti iliyopo wilaya ya Ilala na shule ya sekondari Mbagala iliyopo wilaya ya Temeke ambapo kila shule imepata vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.


Akiongea wakati wa kukabithi vitabu hivyo, Meneja huduma kwa jamii Airtel Bi Hawa Bayumi alisema”  Tunayofuraha kuendelea na mpango huu wa “shule yetu”  kwa mwaka huu na kuwa na shule mpya zitakazofaidika na vitabu vya masomo ya Sayansi. Tunazo shule zaidi ya 30 ambazo tumezipata kwa kushirikiana na uongozi wa serikali zitakazofaidika na msaada huu wa vitabu kwa mwaka huu,  Na leo tumeweza  kuzifikia shule za Kambagwa, Mvuti na Mbagala na kuwapati  vitabu vitakavyoweza kuleta tija katika ufaulu na elimu kwa ujumla”.


“Nia yetu ni kuendelea kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu katika kuinua sekta ya elimu nchini huku tukiwekea mkazo katika masomo ya sayansi kwani tuaamini ulimwengu na nchi inahitaji wanasayansi wengi ili kwenda na kasi ya ukuaji wa technologia. Natoa wito kwa walimu na wanafunzi basi watumie vitabu vizuri na kuweza kuongeza wanafunzi wengi katika masomo ya sayansi na hatimae kuongeza ufaulu zaidi.aliongeza” Bayumi


Akiongea kwa niaba ya walimu wakuu wa shule zilizopokea msaada jijini Dar es saalam, Mwalimu mkuu wa shule ya Mbagala Bi Marcelina  Kimaro alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa  kutufikia leo, tumekuwa tukiona shule nyingi zikifaidiaka na mpango huu wa “Shule yetu” na leo tunayofuraha kupokea msaada wa vitabu vya  Hisabati, Chemia, physikia na Baiologia kutoka Airtel


Shule hii ya mbagala Sekondari ina jumla ya wanafunzi 2031 na uwiano wa vitabu kwa wanafunzi kwa sasa ni kati ya kitabu kimoja kwa wanafunzi wa 3 au 4 , kwa msaada huu leo utasaidia kupunguza

changamoto tuliyonayo ya uhaba wa vitabu na kufanya uwiano kuwa kitabu kimoja kwa wanafunzi wawili. Halikadhalika msaada huu utatupatia urahisi katika kusoma na walimu kuandaa masomo yao.


Kimaro aliongeza kwa kusema” Vitabu hivi vimetupa changamoto  kubwa ya kuongeza juhudi katika masomo kwani nyenzo sasa tunazo na tunaamini wanafunzi wetu wa masomo ya sayansi watasoma kirahisi na hatimaye kupata  idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi.Tunawaahidi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa faida ya wanafunzi na jamii kwa ujumla” Chini ya mpango wa “shule yetu” Airtel imeweza kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari zaidi ya 1000 nchini huku mpango ukiwa ni kizifikia shule nyingi zaidi kila mwaka

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Airtel Donate Books to Secondary schools in Dar

· It through shule yetu program, more than 30 schools to benefit from books aid this year


Airtel Tanzania through “shule yetu” program has donated scholastic materials to 3 secondary schools in Dar es Salaam. This aid is continuation of Airtel’s effort to support education sector in the country.

The 3 beneficiaries schools are Kambagwa Secondary school in Kinondoni District, Mvuti Secondary school in Ilala District and Mbagala Secondary school in Temeke District, were each school will receive education books worth 1.5Million shillings.

Speaking during handover ceremony, Airtel Social Responsibility Manager Hawa Bayumi said” we are glad to have new set of schools that were identified through local authorities and our zonal business managers. Since the establishment of Shule yetu project we have so far reached more than 1000 secondary schools countrywide and today we are happy to extend our support to Kambagwa, Mvuti and Mbagala secondary schools in Dar.”


Our Aim is to collaborate with government through Ministry of education to continue to supporting the sector. Focusing on sciences, it is imperative that we equip our youth to become the catalyst for development in our country recognizing we live in a world of ever growing technology.” Added Hawa.  Through our sustainable project “shule yetu”,  Airtel will continue with it role of facilitating books to schools with shortage of teaching materials and increase level of performance in most secondary schools in general.


Speaking on behalf of other beneficiary schools, Mbagala secondary Head mistress Marcelina. P. Kimario said” we thank Airtel for reaching us today,  we have seen many schools benefiting from Airtel Shule Yetu in the past and we were anxiously waiting for our turn, and we are glad that Airtel has reached out to us through this project.


The school has total number of students 2031 and the current book ratio is at 1 book for 3 to 4 students, with this aid we will have book ration at 1 per 2 students. Additional the books aid will facilitate easy learning and set a good challenge for our students to put more effort in their studies in order to perform better. 

We promise to effectively use the books for the betterment of the students and the community as a whole. Added Mrs. Kimario.

No comments: