Mama Salma Kikwete |
Na Anna
Nkinda – Maelezo
Ili
kuhakikisha vifo vya kina mama wajawazito vinapungua ni lazima wajifungue
katika mazingira salama huku kukiwa na upatikanaji wa kutosha wa vifaa tiba.
Hayo
yamesemwa jana na Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mama Salma Kikwete
wakati akiongea na viongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) iliyopo Keko Jijini Dar es
Salaam.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
alitembelea makao makuu ya MSD kwa ajili ya kuangalia vifaa tiba ikiwa ni
pamoja na vifaa vya kujifungulia kina
mama wajawazito.
Alisema
kama mama atajifungua katika mazingira salama nchi itaweza kuvuka malengo ya
milinia ya kupunguza vifo vya kina mama wajawazito ambavyo kwa sasa vimepungua
kutoka 452 kwa kila vizazi hai 100000 hadi kufikia 432 kwa kila vizazi hai
100000 jambo ambalo litasababisha maisha ya mama kuwa bora.
“Moja
ya kazi zinazofanywa na taasisi ya WAMA ni kuboresha afya ya mama na mtoto hapa
nchini, katika hili tunatoa vifaa tiba vikiwemo vitanda vya kujifungulia kina
mama wajawazito katika Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati ili kuhakikisha kina mama wanajifungua
katika mazingira salama” .
Wakati
wa ziara ya Rais Kikwete mkoani
Morogoro niliahidi kutoa vitanda vya kujifungulia ili kina mama waweze
kujifungua salama, nimekuja hapa na nimejionea vitanda vizuri na vya kisasa vya
kujifungulia pamoja na vifaa vingine ambavyo vinatumika kwa mama mjamzito
naahidi nitawapelekea vifaa hivyo”, alisema Mama Kikwete.
Aidha
Mama Kikwete pia aliwataka viongozi hao kuongeza juhudi katika utendaji wao wa kazi ya kuokoa maisha ya binadamu na
kuhakikisha dawa wanazozipokea zinafika kwa mlaji kwa wakati kwani kama
zitafika kwa wakati vifo vitapungua.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Cosmas Mwaifwani alisema tangu mwaka
wa fedha uliopita wameanza kupeleka dawa na vifaa tiba moja kwa moja katika
ngazi ya vituo vya afya na kuvifikisha kwa mlaji nia ikiwa ni kufikisha huduma
hii kwa mlengwa kwa ubora unaotakiwa na kwa wakati.
“Dhina
ya MSD ni kuwezesha
upatikanaji wa vifaa tiba vyenye ubora kwa bei naafuu kwa watanzania wote,
ndiyo maana tunafika Tanzania nzima na hata kule ambako kuna ugumu wa kufika
zinaangaliwa njia mbadala za kufika huko”.
Hivi
sasa tunaweza kusimama na kuizungumzia dhina hii bila wasiwasi kwani kwa sasa
tafiti zinaonyesha kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeongezeka kutoka
asilimia 45 hadi kufikia asilimia 85”, alisema Mwaifwani.
Alisema
pamoja na kwamba MSD inashughulikia Hospital, Zahanati na Vituo vya afya vya
Serikali na taasisi zilizoidhinishwa na wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bado
ipo tayari kutoa huduma kwa makundi
mengine ambayo yanatuma maombi kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa matumizi ya
wananchi.
Mwaifwani
alisema, “Pale ambapo kundi la watu ama mtu binafsi anapohitaji vifaa tiba kwa
ajili ya matumizi ya wananchi na vifaa hivyo vikiwepo MSD, hatutakuwa na hiyana
ya kutompatia huduma hiyo kwani tumedhamiria kuokoa maisha ya watanzania”.
Bohari
ya Dawa ni moja ya Idara inayojitegemea chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii inajiendsha chini ya Bodi ya wadhamini yenye majukumu makuu matatu ambayo
ni kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara
kwa Hospitali za Serikali na zile zilizoidhinishwa na wizara.
No comments:
Post a Comment