Meneja wa Kanda ya Kusini, Bw, Straton Mushi akitoa maelezo ya muonekano wa duka jipya la Airtel mkoani Mbeya kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Dkt, Norman Sigalla na wanahabari. |
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa AirtelTanzania Bi Adriana lymaba (kushoto) akielezea jinsi duka jipya la Airtel mkoani Mbeya mjini litakavyofanya kazi. |
Mkuu wa wilaya wa Mbeya mjini Dkt Norman Sigalla akilishwa keki na Meneja wa duka la Airtel Mbeya mjini Bi Josephine Mwaimu mara baada ya kukata uzinduzi. |
Wataalam watoa huduma kwa wateja wa Airtel Mbeya mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja. |
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Airtel imeshauriwa
kuongeza maduka makubwa ya kutolea huduma, maeneo ya vijijini , kama
ilivyo kwa maeneo ya mijini, ili kutoa fursa na kurahisisha huduma
kwa wananchi ambao ni vigumu kufika mijini.
Ushauri huo ulitolewana Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dk Norman Sigala, wakati
akifungua duka kubwa na la kisasa la kampuni hiyo Jijini Mbeya , sambamba
na kuipongeza kwa kuwa karibu na wateja wake, na hasa kwenye suala
la utoaji wa huduma za kibenki.
Alishauri wajenge maduka hayo maeneo ya Vijijini, ambako wananchi wengi
hawapati fursa ya kupata huduma kama hizo, na kudai kuwa huduma nyingi za
kibenki zimejikita zaidi maeneo ya mijini pekee.
“ Najua uongozi wa Airtel ni sikivu sana, nawaomba duka kama hili mngefungua na
maeneo ya Mbeya Vijini,naona mengi yako mjini tu,kule vijijini huduma kama hizi
hakuna,najua mmenisikiliza na natarajia matunda mazuri kutoka kwenu”Alisema
Mkuu huyo wa Wilaya.
Aliwataka wananchi kutumia fursa hizo ambazo ni adimu , huku akiipongeza
Kampuni ya Airtel kwa kuboresha duka hilo, na kutoa huduma nzuri kwa
watanzania, jambo ambalo alisema ni mfano wa kuigwa na makampuni mengine.
“ Mimi ni mteja mzuri sana wa hii kampuni,mara nyingi sana huwa nakuja kwenye
hili duka ,lakini jinsi mlivyo liboresha nilitaka kupotea hongereni sana”
Alisema.
Kwa Upande wake Meneja wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu bw, Straton Mushi
alisema mbali na kukarabati duka hilo, pia wameboresha huduma mbalimbali
na kuzitaja baadhi kuwa ni pamoja na huduma ya airtel money, na nyingine
ni kuwa na ushirikiano mzuri kati yao na kampuni ya Tigo.
Alifafanua kuwa kwa sasa mteja wa tigo anaweza kupata huduma za fedha kutoka
kwenye mtandao wa Airtel,na wakati huo pia mteja wa airtel anaweza kupata
huduma hiyo hiyo kwenye kampuni ya tigo hivyo kupanua wigo wa
kibiashara.
Nao baadhi ya wateja wa Kampuni ya Airtel akiwemo Moses Makoga na
Theresia Changa waliipongeza kampuni hiyo kwa kuboresha huduma na huku
wengine wakidai kuwa hawana sababu ya kufungua akaunti za akiba kwenye taasisi
nyingine za kifedha .
“Yaani kwa kweli huduma hapa ni nzuri sana, tukija wanatupokea vizuri sana nahudumiwa utafikiri uko hospitali binafsi
sioni sababu ya kwenda kwenye mabenki na kupanga foleni” Alisema Moses Makoga.
No comments:
Post a Comment