Dar es Salaam
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limesogeza tarehe ya kufanyika kwa mashindano ya ngumi ya Taifa na sasa yatafanyika kuanzia tarehe 03-08/11/2014 Dar es salaam.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika tarehe
08-14/10/2014 Dar es salaam.
Sababu za kusogeza mashindano hayo ni kuyapisha mashindano ya ngumi ya kimataifa yaliyoandaliwa na chama cha ngumi wilaya ya Temeke yanayotarajia kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, lakini pia ni kutoa nafasi zaidi kwa mikoa ili kujiandaa vizuri na kufanya mashindano ya kuwapata wawakilishi wa mikoa yao katika mashindano ya taifa.
BFT tunawataki maandalizi mema na tunatoa wito kwa maafisa michezo wa mikoa yote ya Tanzania bara kuhakikisha wanaleta wachezaji kutoka katika mikoa yao ili kuleta upinzani utakaopelekea kupata timu ya taifa iliyo bora kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara.
Aidha BFT inawapongeza kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kwa udhamini wa mashindano hayo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 10,000,000/=ambazo zitasaidia baadhi ya mahitaji ya msingi ya kufanikisha mashindano hayo.
Imetolewa na:
Makore mashaga
KATIBU MKUU
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mashindano ya Ngumi ya Wavuvi Boxing Tournament kufanyika Septemba 13, Bagamoyo
Dar es Salaam
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limeaandaa
mashindano ya ngumi ya wavuvi Boxing TOUNAMENT yatakayoanza kufanyika tarehe
13/09/2014 katika fukwe za Bagamoyo na baadaye kuendelea katika fukwe
mbalimbali.
Lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha jamii ya wavuvi na watu wanaowazunguka
kujishughurisha na masuala ya michezo na hasa mchezo wa ngumi baada ya shughuri
zao za uvuvi na kuwafanya kuondokana na vitendo viovu vinavyotokana na utumiaji
wa vilevi mbalimbali kupita kiasi na zaidi kuvumbua vipaji kutoka katika jamii
hiyo ikiwa pamoja na kuwapa burudani.
Katika utafiti uliofanywa na BFT tumegunduwa kuwa
katika jamii ya wavuvi wapo wengine wanaopenda michezo hasa mchezo wa ngumi hii
ni kutokana na asili ya kazi yao ya uvuvi ya kutumia nguvu za mikono kwa ajili
ya uvuvi na akili nyingi hivyo tumeazimia kuanza kuwafikia kwa vitendo kwa
kufanya mashindano katika maeneo yao ili kuwahamasisha kijiingiza zaidi katika
michezo.
Mashindano hayo yatakuwa yanafanyika kila siku ya
jumamosi kwa fukwe mbalimbali za bahari
ya hindi na baadaye kuhamia katika fukwe za maziwa makuu.
Mashindano haya yamedhaminiwa na kampuni ya Sam &
Anzai Boat Builder C.,Ltd kwa kushirikiana na C&G
Imetolewa na:
Makore Mashaga
Katibu Mkuu
No comments:
Post a Comment