Umakini
katika kutambua rangi akiuhusisha huyu ni mshindi wa kwanza wa shindano
la Beer Tasting Competition kwa wanahabari (Muonjaji Bora wa Bia) Aidan
Mhando wa Mwananchi Communications akizibainisha bia katika ungwe ya
pili ya na ya mwisho ya shindano hilo.
|
Awali
kabla ya shindano la uonjaji bia, Mpishi mkuu wa Kampuni ya Bia TBL
tawi la Mwanza Oscar Kilasi alitoa somo kwa waandishi hao juu ya
kuzibaini tofauti za bia kupitia ladha, rangi, harufu na viwango vya
alcohol.
|
Kupitia
Big screen hivi ndivyo somo la uonjaji bia lilivyokuwa likiendeshwa ndani ya ukumbi wa mikutano TBL Mwanza.
|
Kupitia
Big screen hivi ndivyo somo la uonjaji bia lilivyokuwa likiendeshwa
ambapo hapa bia aina ya Castle Light ilikuwa ikitolewa maelezo ya
vihusishi vilivyohusika hadi ukamilifu wake na maelezo ya viwango vyake.
|
Kupitia
Big screen hivi ndivyo somo la uonjaji bia lilivyokuwa likiendeshwa
ambapo hapa bia ya Safari Lager ilikuwa ikitolewa maelezo ya vihusishi
vilivyohusika hadi ukamilifu wake na maelezo ya viwango vyake.
|
Bia mbalimbali zinazo tengenezwa na TBL Tawi la Mwanza.
|
Philbert
Kabago (mbele) akiongoza Waandishi wenzake wa habari kutembelea vitengo
mbalimbali vya uzalishaji bia kupitia kiwanda cha kutengeneza bia TBL
kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
|
Waandishi
wa habari wakipata maelezo ya namna ya upikaji bia kupitia kiongozi wa
kitengo cha maabara kiwanda cha kutengeneza bia TBL
kilichopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
|
"Hii ndiyo maabara ya TBL Mwanza"
|
Mtaalamu
wa Ubora wa Bia kiwanda cha TBL Mwanza, David Keregeseni akitoa maelezo
kwa waandishi wa habari William Bundara wa RFA (katikati) na Wilson
Elisha wa Star Tv (kulia) ndani ya maabara ya kiwanda hicho kilichopo
wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
|
Shughuli za uzalishaji zikiendelea ndani ya kiwanda cha kisasa cha kuzalisha bia TBL Mwanza.
|
Blogger Gsengo ndani ya mjengo wa uzalishaji bia Kampuni ya TBL Mwanza.
|
Blogger William Bundala aka Kijukuu cha Bibi ndani ya mjengo wa uzalishaji bia Kampuni ya TBL Mwanza.
|
Uzalishaji ukiendelea ndani ya mjengo.
|
Chupa zikiwa kwenye mstari kuelekea njia ya usafishaji ndani ya mjengo wa uzalishaji bia Kampuni ya TBL Mwanza.
|
Wakiwa shughulini hawa ni wataalamu kitengo cha uwekaji lebo za bia ndani ya mjengo wa uzalishaji bia Kampuni ya TBL Mwanza.
|
Philbert Kabago wa Passion Fm kikazi zaidi katika shindano la Muonjaji Bora wa Bia kiwandani TBL Mwanza.
|
Mashaka Bartazar anayeandikia magazeti ya Majira na Jambo leo akifanya yake.
|
Harufu na uonjari ni sehemu ya kubaini aina ya bia.
|
Biskuti maalum ni nyenzo kwaajili ya kufuta ladha ya bia uloionja awali kabla ya kuionja bia nyigine.
|
We Katulanda, unaonjaaaa au unakunywa? Tehe...teee!!
|
Beer Tasting Competition.
|
Meneja
Mawasiliano na Habari wa TBL Edith Mushi (kulia) akikusanya karatasi za
mtihani wa shindano la Uonjaji bia kwa waandishi wa habari.
|
Meneja
msaidizi katika uzalishaji kampuni ya bia TBL Mwanza, Jemedari
Waziri akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la Beer Tasting
Competition kwa wanahabari (Muonjaji Bora wa Bia) ambapo Aidan Mhando wa
Mwananchi Communications ndiye aliyeitwaa nafasi hiyo kwa mwaka huu
2014-2015.
|
Carolyne
Mhonoli ambaye ni Meneja ubora wa bia wa TBL Mwanza, akikabidhi zawadi
kwa mshindi wa pili wa
shindano la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Fredrick
Katulanda ambaye ni Mhariri wa magazeti ya New habari Kanda ya Ziwa,
katika hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika kiwanda hicho
kilichopo Ilemela mkoani Mwanza.
|
Afisa
Habari na Matukio TBL Mwanza, Mr. Erick akimkabidhi zawadi mshindi wa
tatu wa shindano la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia)
Philbert Kabago wa Passion Fm Mwanza, katika hafla fupi iliyofanyika
mwishoni mwa wiki katika kiwanda hicho kilichopo Ilemela mkoani
Mwanza.
|
Kila mmoja alitoka na zawadi yake.
|
Mzigo umeuonaaaa!!?
|
Bia tayari kwa kuingia sokoni.
|
Tukipata U-PichaZ.
|
Wanyama.
|
Picha
ya
pamoja ya waandishi wa habari na wadau wa TBL mara baada ya kumaliza
matembezi katika kiwanda cha Tanzania Breweries Limited Mwanza.
|
MPANGO MZIMA KWA UFUPI.
MWEZI wa
Sita wa kila mwaka kampuni ta Tanzania Breweries Limited (TBL) inaandaa
mashindano kwa waandishi wa habari kwa ajili ya kubaini vinywaji vya
kampuni hiyo kwa kuonja ladha tofauti kisha kutambua ni bia gani.
Jijini
Mwanza mashindano hayo yamefanyika jana katika kiwanda cha TBL na
kushirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari zaidi ya Ishirini kutoka
vyombo mbalimbali vya habari jijini mwanza.
Katika
mashindano hayo yaliyodumu takribani dakika thelathini yalimalizika kwa
waandishi watatu kulingana point hali iliyopelekea mchuoano kurudiwa
kwa watu watatu ili kumpata mshindi.
Katika
marudio hayo mwandishi na Mtangazaji wa kituo cha Passion Fm Filbert
Kabago aliibuka mshindi wa tatu hali iliyopelekea kutafuta mshindi wa
kwanza na pili kati ya mwandishi wa gazeti la mwananchi Aidan Muhando na
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania Fedrick Katulanda.
Baada
ya kupambana Aidan Mhando aliibuka mshindi wa kwanza na Fedrick
Katulanda akakamata nafasi ya pili. Baada ya mashindano hayo waandishi
walipata nafasi ya kutembelea eneo la maabara na eneo la uzalishaji ili
kujionea namna bia za kampuni ya TBL zinavyozalishwa na kupata nafasi ya
kuuliza Maswali ili kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii.
Licha
ya kubainisha kuwa ziara hiyo imesaidia kutambua masuala ya biashara
takayo saidia kufikisha ujumbe kuhusu bidhaa zinazo zalishwa na kampuni
hiyo, mmoja wa waandishi wa Clouds Fm jijini Mwanza ambaye pia ni
mmiliki wa G.Sengo Blog, Albert Sengo amesema ziara hiyo ya wazi kwa
waandishi wa habari ambao ni wadau wa kuibua taarifa na changamoto
zilizopo ndani ya jamii, ni ushahidi tosha kwamba kiwanda hicho cha
kutengeneza bia kinajiamini katika masuala yote ya teknolojia, afya,
usafi na uzalishaji makini, kwani kungekuwa na magumashi (ubabaishaji)
basi TBL wasinge thubutu kuwapa uhuru wadau hao kujiachia katika kuuliza
maswali na kunasa matukio mbalimbali kiwandani humo.....
No comments:
Post a Comment