Msanii
wa Bongo Movie, Kajala Masanja (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dare s Salaam jana, kuhusu ushiriki wake katika tukio la uoshaji
magari linalojulikana kama “Celebrities
Charity Car Wash” lenye lengo la kuchangia fedha Wodi ya Dharura katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, litakalowashirikisha watu maarufu wakiwemo
wasanii nyota wa filamu nchini, litakalofanyika wakati wa Tamasha la Magari
Auto Fest 2014, Septemba 20 mwaka huu katika Viwanja vya Biafra Kinondoni
jijini Dar. Kutoka (kushoto) ni Msanii nyota wa Bongofleva na Mkurugenzi wa
Jaffarai Car Wash, Jaffai Msham, Msanii wa Bongo Movie, Jenefer Kyaka ‘Odama’
na Msanii Blandina Chagula ‘Johari’.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Dar es Salaam.
Masupa
staa wa Tanzania wathibitisha ushiriki wao katika “Celebrities Charity Car Wash” litakalo fanyika sambamba
na tamasha la Auto Fest 2014. Linatarajiwa kufanyika tarehe 20th
September, 2014 katika viwanja vya Biafra Kinondoni, Dar es Salaam.
Waliosibitisha
ushirki wao ni Irene Uwoya,Odama, Kajala Masanja, Monalisa, Aunty Ezekiel, Lulu
Michael, Johari, JB, Ritchie.
Tamasha
hili kwa mwaka huu litajumuisha
“Celebrity Charity Car Wash” ikiwa ni njia moja wapo yakutoa hamasa kwa
wananchi kuchangia wahanga wa ajali nchini. “Kutokana na matukio mengi ya ajali
nchini tumeona nakutambua kuwa wengi wa majeruhi hutibiwa bure basi ni vyema
tukaandaa tukio linalo husiana na tamasha letu wakati huo huo tukiweza
kuchangia mahitaji muhimu katika wodi hizi”. Alisema Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa
Vision Investments. “Tunarajia watu watahamisika kukemea madereva wanao tumia
barabara vibaya tukielekea katika wiki ya usalama barabarani.
Tukio
hili linalenga kuchangisha fedha kwa mfumo wa kuosha magari kwa bei
yakuafikiana na Supa staa “CELEBRITY”.
Tunakaribisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika uchangiaji huu.
Lengo letu kwa mwaka huu likiwa nikuchangia Wodi ya Dharura katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (Emergence Medicine Unit).
Burudani kwenye tukio zitahusisha, Gari lililo pambwa (Pimped) ambayo ni nafasi
kwa wapenzi wa magari kuonyesha walivyoyapamba magari yao, Bingwa wa misele,
Bingwa wa 4x4, B-Boy Dance, ‘Kids Car Zone,’ ambayo itawaburudisha watoto wa
umri kati ya miaka mitano na 14 kwa program za magari na elimu muhimu ya magari
na usalama barabarani, na kuweza kuburudika na mbinu mbalimbali za kuchezesha
magari kama norinda “misele”.
Tamasha la Autofest
mwisho wa wiki linategemea kuvutia watu wengi,
na kulifanya kuwa tamasha kubwa na maarufu la magari Tanzania likiwa katika
mwaka wake wa saba.
Kushiriki katika
maonyesho ya mwaka huu tembelea mtandao wa www.autofest.co.tz.
No comments:
Post a Comment