Tangazo

September 15, 2014

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA SHIRIKA LA HEIFER INTERNATIONAL STEVE DENNE NCHINI

DSCN1621
Mfugaji wa Heifer International Tanzania Abel Mwakatumbula na mkewe wakiwa na Makamu wa Rais wa shirika hilo.

Steve Denne alitembelea Tanzania kwa mara kwanza wiki iliyopita kuona miradi inayoendeshwa na shirika hilo.

Katika ziara hiyo, Steve Denne alitembelea ofisi za mkoa wa Mbeya akifuatana na Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Dk Henry Njakoi, Meneja Mradi wa EADD Tanzania Bwana Mark Tsoxo, ambapo walikutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro. 

Katika Mazungumzo yake na Mheshimiwa Abbas Kandoro, Bw Denne aliishukuru sana serekali ya Tanzania kwa mahusiano mazuri na ushirikiano mkubwa kwenye kutekeleza miradi ya shirika hilo nchini na hasa katika kuanzisha Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD). 

Aliahidi kuwa shirika hilo kupitia mradi wa EADD na miradi mingine tarajiwa, litaendelea kuleta mabadiliko kwa kuwasaidia wafugaji wadogo kwenye mikoa wa Mbeya, Iringa na Njombe ili kuinua uchumi wao na kuwa na ufugaji wenye tija na endelevu.

Pamoja na miradi aliyoitembelea Steve Denne, mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) unaoanza Mkoani Mbeya wilaya ya Rungwe kijiji cha Kyimo ambapo aligawa mtamba kwa mfugaji wa kikundi cha Faraja kama dira ya shirika hilo ya “Toa Zawadi Pia” – Pass On The Gift.

Akiwa nchini, Makamu wa Rais wa shirika la Heifer International alikutana na wadau mbalimbali wa sekta ya maziwa nchini wakiwemo wasindikaji, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar ambapo alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Kassim Gharib Juma.
DSCN1660
Makamu wa Rais wa Heifer International Steve Denne, Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Dk. Henry Njakoi wakifurahia mafanikio ya miradi ya Heifer International.
DSCN1799
Makamu wa Rais wa Heifer International akigawa mtamba kwa mwana kikundi cha Faraja Wilayani Rungwe.
DSCN1908
Steve Denne akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Abbas Kandoro alipotembelea ofisi za Mkoa.
DSCN1909
Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne, Meneja Mradi wa EADD Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika picha ya pamoja.
DSCN2098
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana akiwakaribisha ofisini kwake, Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne na Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania Dk. Henry Njakoi.
DSCN2100
Steve Denne alipomtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana.
DSCN2111
Steve Denne katika mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana.
DSCN2320
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dk. Kassim Gharib Juma (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne na Dk. Henry Njakoi, Mkurugenzi wa Shirika hilo nchini.

No comments: