Tangazo

October 20, 2014

FACEBOOK KUTUMIKA KUFUNZA USALAMA BARABARANI

DSC_0135
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (wa pili kushoto) akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Kushoto ni Mratibu wa Mradi wa kuboresha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (wa pili kulia) nje ya ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Na mwandishi wetu, Dodoma

Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, amekubaliana na haja ya kuanzisha mafunzo katika vyombo vya habari vya kijamii kama facebook ili kutanua uwanja zaidi wa elimu ya usalama barabarani hasa kwa vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa ajali.

Aidha amesema Polisi wanafikiriia kuanzisha mfuko wa kielektroniki wa ulipaji wa faini kwa makosa ya barabarani ili kuongeza kasi ya udhibiti na kuondoa tuhuma za rushwa.
Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanahabari na watendaji kutoka redio za jamii nchini mjini Dodoma, katika warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP).

washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
DSC_0141
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph, akisalimiana na Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, mara baada ya kuwasili kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

Kauli yake hiyo ilifuatia hoja iliyotolewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO), Bw. Al Amin Yusuph, ambaye aligusia redio za jamii katika kusambaza habari zenye kulenga kuokoa maisha na mali kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Mpinga ambaye pia ni kamanda wa kikosi cha usalama barabarani alisema katika mada yake kwamba changamoto kubwa ni kutekeleza sera ya kuhakikisha kwamba hakuna kifo wala majeruhi katika ajali za usalama barabarani.

Akielezea hali halisi ya ajali barabarani huku akikariri takwimu za Benki ya Dunia na Shirika la Afya Duniani (WHO) kamanda Mpinga alisema kwamba utafiti unaonesha katika kila wakazi 100,000 duniani 24 hufa katika ajali za barabarani ambapo vijana na watu maskini ndio wapo katika hatari kubwa zaidi.

Aidha alisema takwimu zaidi kutoka WHO zinasema kwamba watu million 1 na laki tatu hufa kila mwaka duniani hapa kwa ajali huku ikibainisha kwamba asilimia 75 ya watu wanaojeruhiwa na kufa wanatoka katika nchi maskini ambazo hazina magari mengi kama zile zilizoendelea.
DSC_0171
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph (kushoto) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, kutoa mada kwa watendaji wa redio za jamii nchini. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Meneja wa redio jamii Sengerema FM ya mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.

Alisema pamoja na takwimu hizo za kutisha za duniani, nchini kwetu pekee watu 4000 hufa kila mwaka kutokana na ajali na mwaka uliopita walikufa watu 4002.

Akitoa mada katika mafunzo hayo alisema kwamba ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa na binadamu ambapo asilimia 75 za ajali zote husababishwa na makosa ya kibinadamu.

Alisema utafiti unaonesha kwamba makosa hayo chanzo chake ni uzembe, ulevi, mwendo kasi, kutozingatia sheria, uchovu wa madereva na matumizi ya vyombo vya moto.
Aidha uzembe wa waendesha pikipiki ndio unabeba asilimia 20 hadi 30 ya ajali zote.
Alisema kufunguliwa kwa biashara ya pikipiki kubeba abiria kumewaingiza vijana wengi ambao wengi wao si wataalamu wakikosa sifa ya kuendesha vyombo hivyo vya moto huku wakiwa vinara wa kuvunja sheria barabarani kwa vitendo.
DSC_0212
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akiwasilisha mada kwa watendaji wa redio jamii nchini (hawapo pichani) waliokuwa wakihudhuria warsha ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo (UNDP) iliyoamlizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Meneja wa redio jamii Sengerema FM ya mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.

Madereva hao alisema wanaendesha kasi, hawavai kofia ngumu na kubeba abiria kwa mtindo wa mishikaki.

Akifafanua zaidi amesema kwamba pamoja na madereva wa pikipiki kuongoza kwa kuvunja sheria hali za barabara kama kukosekana kwa alama, muundo wa barabara zenyewe, utelezi , uchakavu wa vyombo na hali ya hewa vimekuwa visababishi vya ajali.

Kamanda alitaka vyombo vya habari vya redio za jamii kuelimisha madereva matumizi sahihi ya barabara kwa kuwaita wataalamu kuelezea mambo hayo bila chumvi wala kuharibu nidhamu na maisha .

Alisema mathalani maeneo ya mnadani madereva wamekuwa wakivunja sheria hasa upakiaji wa mizigo isiyozingatia usalama wa abiria waliomo.

Alisema jeshi la polisi limechukua mikakati kadhaa kuwezesha kukabiliana na hali ya usalama barabarani hasa kwa kuanzisha ukamataji wa makosa hatarishi katika usalama wa barabara.
Makosa hayo ni mwendokasi, ulevi, uendeshaji wa hatari na uzidishaji wa abiria alisema faini zinazotolewa zimefanya kupungua kwa ajali kutoka elfu 17 hadi elfu 11.

Alisema mikakati mingine ni utoaji wa elimu kwa kupitia vyombo vya habari na kushukuru kwamba elimu hiyo anaona inasaidia. Alisema wanatoa elimu kupitia televisheni , redio na vyombo vya habari vya kijamii.
DSC_0196
Aidha wamekuwa wakishiriki kutoa mafunzo wakishirikiana na wadau wengine.
Pia aliutaja mkakati mwingine ni kuboresha mifumo ya utendaji kwa kuainisha maeneo yanayotokea ajali mara kwa mara, ukusanyaji wa takwimu na kubadili mfumo wa ukaguzi barabarani kwa kuanzisha maeneo maalumu ya kukagulia magari kwa undani.

Pia kunatengenezwa mfumo wa nukta ambapo dereva anapofanya makosa pointi zinaondolewa na zikimalizika anapokonywa leseni.

Kuhusu ulipaji wa faini kupitia benki na njia nyingine za elektroniki alisema zitarahisha utendaji wa polisi na kuondoa tuhuma za rushwa na pia kuwafanya watu kuwa waangalifu zaidi.

Aidha amesema wanatengeneza utaratibu kwa kushirikiana na wadau wengi kutengenezwa kanuni ya ulazima wa madereva kurejea shule kwa mafunzo hasa kutokana na kubadilika mara kwa mara kwa miundombinu ya barabara na teknolojia ya magari.
DSC_0200
Sehemu ya wadau/watendaji wa redio jamii wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha Demokrasia na Amani nchini (DEP) kuelekea uchaguzi mkuu ujao wakifuatilia kwa umakini mada iliyowasilishwa na Kamanda Mpinga kwenye warsha hiyo.

Hata hivyo alisema pamoja na mikakati hiyo na mingine Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto zinazoambatana na bajeti ndogo ya kuiwezesha kununulia vifaa vya kazi kama speed radar za kisasa na mifumo muafaka ya kusimamia usalama barabarani ambapo kwa sasa kila tatizo wanasukumiziwa polisi iwe ni taa mbovu za barabarani au mashimo.
Changamoto nyingine ni wananchi wenyewe kukosa utamaduni wa kuheshimu sheria mpaka waone polisi.

Alivitaka vyombo vya redio jamii kufundisha wananchi na wala sio kuchochea wao wazidi kuvunja sheria na kuitoa mfano wa matuta barabarani ambayo yanadaiwa na wananchi na kusema hiyo si dawa bali elimu kwa wananchi kuhusu usalama barabarani na namna ya kudhibiti ajali.

Naye Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Unesco , Bw. Al Amin Yusuph akimkaribisha Kamanda Mpinga azungumze alisema mafunzo hayo yameandaliwa kwa ajili redio za jamii kujiuza kw apamoja katika kuhudumia umma na kujiendeleza.

Alisema redio ndio njia pekee ya kuwafikia watanzania wengi hasa kwa kuzingatia kwamba watumiaji wa vyombo vingine ni wachache hasa kutokana na kukosekana kwa nishati na pia kuwa mbali na maeneo yanayotangaza habari.
DSC_0221
Wasaidizi wa Kamanda Mpinga wakigawa machapisho mbalimbali yanayotoa elimu ya usalama barabarani kwa washiriki wa warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Dodoma.
DSC_0244
DSC_0240
Reportuer wa warsha ya wadau wanaotekeleza mradi wa uchaguzi iliyomalizikia mwishoni mwa juma mjini Dodoma Mchungaji Privatus Karugendo akihoji suala la baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto wanaotumia simu za viganjani pindi wawapo barabarani kitu ambacho ni hatari kwa usalama wao.
DSC_0268
Baadhi ya machapisho yaliyogawiwa kwa watendaji wa redio jamii nchini yanayotoa elimu ya usalama barabarani.
DSC_0255
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakipitia machapisho hayo yaliyotolewa na Kitengo cha Polisi Usalama Barabarani kwenye warsha hiyo.
DSC_0259
DSC_0287
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipata picha ya kumbukumbu na Mshiriki wa warsha hiyo Prosper Kwigize.
DSC_0292
Naibu Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akifurahi jambo na Mkurugenzi wa redio jamii Uvinza Fm, Alhaji Ayubu Kalufya.

No comments: