Tangazo

October 4, 2014

Twanga Pepeta kutambulisha Lilian Internet na Kaba5 Mango Garden leo


Na Mwandishi Wetu

Bendi ya Twanga Pepeta leo (Jumamosi)  itamtambulisha rasmi mnenguaji wake maarufu Lilian Enternet aliyerejea kundini kwenye onyesho maalum litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni.

Mara ya mwisho Lilian alichezea bendi ya Mashujaa.

Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (Aset) ambayo inamiliki bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema jana kuwa onyesho hilo maalum la kukaribisha sikukuu ya Idd el Hajj pia itatumika kumtambulisha rapa wa zamani wa bendi ya Extra Bongo, Frank Kaba maarufu kama Kaba5 aliyejiunga na bendi hiyo hivi karibuni.

Asha pia amewaomba wapenzi wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi ili wapate burudani inayojumuisha nyimbo mpya na rap mpya kutoka kwa Msafiri Diof.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa Lilian Internet atashambulia jukwaa akishirikiana na wanenguaji wenzake kama Maria Soloma, Sabrina Pazi, Sabrina Kado, Stella George, Vicky Daudi, Aisha Lokole na Fety Kibororoni. Pia wamo Danger Boy, Dogo White, Mada, Dogo Saidi, Mandela.

Safu ya uimbaji itajumuisha Kalala Junior, Saleh Kupaza, Dogo Rama, Luiza Mbutu, Diof, Haji Ramadhani, jumanne SDaid, Rama Pentagon, Frank Kaba na Badi Bakule.

Alisema bendi hiyo ijulikanayo kama Wakali wa Kisigino pia watapiga nyimbo zao zote kali hadi majogoo.

Onyesho hilo limeandaliwa na Keen Arts na kudhaminiwa na Konyagi, CXC Africa na Nevada Barber Shop.

No comments: