Tangazo

October 6, 2014

NSSF FURSA SEMINA DODOMA YASHAMIRI SIKU YA IDD EL HAJJ

 Ikiwa ni muendelezo wa Semina za Fursa zinazoendelea katika mikoa mbalimbali, licha ya kuwa ni Siku ya Sikukuu ya Idd El Hajj, Fursa Semina ilishamiri mjini Dodoma na kuvutia umati mkubwa wa watu.

Umati huo ulivutiwa na huduma na mafao yatolewayo na NSSF kama vile Matibabu Bure kwa mwanachama na wategemezi wake, mikopo kupitia Saccos, Mafao ya kuumia kazini, Pensheni ya Uzeeni, Pensheni ya Urithi, Msaada wa Mazishi na Pensheni ya Ulemavu.

NSSF iliwasihi watu wajiunge na mfuko huo ili waweze jipatia Fursa za kuboresha maisha yao ya sasa na ya baadae.

Semina ya Fursa Dodoma ilirushwa Live na kituo cha Redio cha Clouds FM katika mkoa wa Dodoma  na hivyo kuwapa Fursa hata wale walioshindwa kufika ukumbini kufuatilia mada mbalimbali zilizotolewa popote walipo ndani ya mkoa huo.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa kwanza kulia), Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma,  Kirondera Nyabuyenze (wa pili kulia) na Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba  (wa tatu kulia) wakiwa katika semina ya Fursa Dodoma.
 Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume (wa tatu kushoto) na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Kirondera Nyabuyenze (wa pili kushoto) wakifutilia kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa katika semina ya Fursa Dodoma.
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akitoa mada katika Semina ya Fursa Dodoma. 
 Baadhi ya watu waliohudhulia semina hiyo wakiskiliza kwa makini Fursa zitolewazo na NSSF.
Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa watu waliohudhuria semina hiyo.
 Mwanamuziki wa kizazi kipya Mwasiti Almasi akiwahamasisha wananchi waliohudhuria semina hiyo wajiunge na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili waweze jipatia Fursa za kuboresha maisha yao ya sasa na ya baadae. Kushoto ni Ofisa wa NSSF, Ally Mkulemba 
 Maofisa wa NSSF, Gabriel Nkakatisi (kushoto) na Anna Nguzo wakiandikisha wanachama wapya baada ya kumalizika kwa semina ya Fursa iliyofanyika siku ya sikukuu ya Idd El Hajj mjini Dodoma.
Baadhi ya watu wakijiandikisha katika banda la NSSF baada ya semina ya Fursa Dodoma. 

No comments: