Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akionyesha
kadi maalum ‘Premier Card’ aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel
Tanzania, Sunil Colaso (kulia), baada ya kuzindua Mpango Maalum wa Airtel kwa
wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za
hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi
asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika
hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imezindua mpango maalumu utakaowawezesha wateja
wake wakubwa kufurahia huduma za ziada wawapo kwenye kazi
zao. Mpango huu wenye lengo la kuwazawadia wateja wa
Airtel utakuwa na kadi maalumu ya kusafirisha yaani (Priority
Pass) itayowawezesha wateja wakubwa wa Airtel kupata huduma ya hadhi
ya juu kwenye viwanja vya ndege duaniani na pia kupata
punguzo la hadi asilimia 30 pindi watakapo nunua bidhaa na kupata huduma nchini.
Kufatia uzinduzi huo wateja wa
Airtel sasa wataweza kuunganishwa na huduma za hadhi ya juu kwenye viwanja vya
ndege zaidi ya 700 duniani na hivyo kupata viburudisho,
urahisi wa huduma yaani (VIP services) pindi wasafiripo na kuwawezesha kufurahia
safari zao.
Sambamba na hilo wateja hao pia
watapata punguzo la hadi asilimia 30 pale watakapopata huduma au kununua bidhaa
katika maeneo mbalimbali ikiwemo hotel, migahawa, maduka makubwa and sehemu
nyingine nyingi.
Akiongea wakati wa uzinduzi Waziri
wa Nchini katika ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary
Nagu alisema” nawapongeza sana Airtel kwa kuzindua mpango huu maalumu na
kuwazawadi wateja na watanzania nchini. Nafurahi kuona pamoja na
changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano lakini bado
tunashuhudia Airtel inajipanga na kujikita katika kuboresha huduma kwa wateja
wake.
Natumaini kadi hizi maalumu
tunazozindua leo zitawaweza watanzania kupata mwanya wa kutengeneza mahusiano
na kutanua wigo wa marafiki wa kibiashara na mwisho kuweza kuvumbua fulsa
mbalimbali za kibiashara duniani.”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Airtel Bwana Sunil Colaso alisema “ kupitia huduma hii tunadhirisha lengo letu
la kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu. Tunauhakika kadi
hii maalumu ya kupata huduma zenye hadhi katika viwanja vya ndege
mbalimbali duniani hazitarahisha safari zao tu bali zitawawezesha
kufanya mahusiano ya muda mrefu ya kibiashara kwa wale watakaokutana nao wakati
wa safari.
Ni matumaini yangu kuwa mpango
huu utaleta tija na kuwapatia wateja wetu unafuu wa kutanua
biashara zao.
Katika halfa hiyo Airtel pia
ilizindua pia huduma yake ya internet ijulikanayo kama Home Wi-Fi
solution, kwa kupitia huduma hii ya Airtel Wi-Fi mteja anaweza kuunganisha
simu zaidi ya 32 katika kifaa kimoja cha Wi-Fi , kuunganisha hadi simu za
mkononi 4 na kuwaunganisha na Wi- Fi ya nyumbani hata kama wakiwa mbali na
nyumbani wakati wote mahali popote nchini. Hii ina maana kwamba sasa wateja wa
Airtel wanaunganishwa na kifaa kimoja cha familia , kwa kupitia kifurushi
kimoja, kupitia huduma hii mpya ya Airtel Wi-Fi.
No comments:
Post a Comment