Tangazo

November 24, 2014

KINANA AHITIMISHA ZIARA KWA KISHINDO LINDI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Lindi Leo, kuhitimisha ziara ya siku 8 katika Mkoa wa Lindi ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Lindi, ambapo amesema wapinzani wajiandae kupigwa mweleka katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa Desemba 2014, akidai hawana mpango wa kuwaletea maendeleo wananchi.Pia amesema Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini Baruani wa CUF, ajiandae kung'oka akidai kodi yake imekwisha.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishishiriki kuchimba  miundombinu ya maji katika Kijiji cha Mingoyo Mnazi Mmoja Lindi Mjini leo
 Kinana akiungana na wananchi kupapalia  katika shamba la kuzalisha mbegu bora za mihogo katika Kijiji cha Chikonji, wakati wa zaiara yake Wilaya ya Lindi Mjini.
 Kinana akisaidia kubeba zege za kujengea nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Nanyanje, Lindi Mjini.
 Kinana akishiriki kuvua samaki katika moja ya mabwawa 12  ya mjasiriamali Mjini Lindi
 Komredi Kinana akipandisha bendera wakati wa uzinduzi wa shina la Wakereketwa la CCM la Wanywaji wa  Kahawa mjini Lindi leo.
 Komredi Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Lindi leo
 Kikundi cha Mangongoti kikitumbuiza katika mkutano huo
 Komredi Kinana akiwapongeza vijana wa Chuo cha Veta walioujiunga na Umoja wa Vijana wa CCM wakati wa mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Ally Mtopa akihutubia kabla ya kumkaribisha Kinana wakati wa mkutano huo.
 Kinana akihutubia umati mkubwa wa wananchi mjini Lindi leo

 Kinana akiwapatia kadi za CCM wanachama waliohama kutoka vyama vya upinzani
 Mwanachama wa CUF kwa miaka 18, Omari Kalunda akitangaza kuachana na chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Ally Mtopa akimzawadia mgolole Komredi Kinana kwa niaba ya wazee wa mkoa wa Lindi

No comments: