Tangazo

November 24, 2014

KALA JEREMIAH AFANYA UZINDUZI WA VIDEO NA AUDIO YA NYIMBO YAKE MPYA YA "USIKATE TAMAA"


 Kala Jeremiah akichana mistari.
Mwanamziki wa Hip hop, Kala Jeremiah amezindua video yake ya Wimbo Usikate Tamaa  aliomshirikisha Nuruwell katika Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Katika uzinduzi huo, Kala alisindikizwa na mastaa kibao wakiwemo Mo Music, Ben Pol, La Veda, Stamina, Ney Lee ambao waliporomosha shoo za nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria uzinduzi huo. Kala Jeremiah amesema audio na video zinatarajia kutoka rasmi siku ya Jumatano yaani tarehe 26/11/2014.(Picha na Pamoja Blog)
   Kala Jeremiah akiendelea kufanya ya kwake kwenye stage wakati wa uzinduzi video 'Usikate Tamaa'.
 Mshiriki wa Big Brother Hotshots, Irene La Veda akionyesha ufundi wa kutumia saxaphone ndani ya Ukumbi wa Miasha Club usiku wa kuamika leo.
 Ney Lee akiimba kwa hisia kali.
 Mo Music akizidi kuwadatisha mashabiki ndani ya Maisha Club.
 Ben Pol akiwapa raha mashabiki wa Maisha Club usiku wa kuamkia leo kabla ya uzinduzi ya video 'Usikate Tamaa'.
 Ben Pol akiendelea kufanya yake stejini.
 tamina akizidi kutiririsha mistari kwa mashabiki wake. 

 Kala Jeremiah akikamua sambamba na Ney Lee kabla ya kuzindua video yake ya Usikate Tamaa.
Ney wa Mitego aliwapa suprise ya nguvu mashabiki waliofika katika uzinduzi wa nyimbo ya Kala kwenye ukumbi wa New Maisha jijini Dar
Kala Jeremiah  akionesha ishara inayotanbulisha maana ya wimbo wake mpya wa "usikate Tamaa"
 Kala akiwatambulisha pia walioshiriki katika video ya wimbo wake huo wa "Usikate Tamaa" aliomshirikisha Nuruwell. Na hivi hapa chini ni vipande vya video ya nyimbo mpya ya Kala Jeremiah 

 Nuruwell akiimba kwa hisia wakati wa uzinduzi wa video ya Usikate Tamaa.
Kala Jeremiah (kushoto) na Nuruwell wakipafomu kwa mara ya kwanza wimbo wa Usikate Tamaa ndani ya Maisha Club.

No comments: