Tangazo

November 21, 2014

AIRTEL YAMWAGA VITABU VYA MILIONI 15 WILAYANI MAKETE –NJOMBE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (katikati), akipokea msaada wa vitabu kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton (kulia), utakaofaidisha jumla ya shule 5 zilizopo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Shule zinazofaidika ni Iwawa, Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana katika shule ya Iwawa iliyopo wilayani Makete. Anaeshudia (kushoto) ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa Shule ya Iwawa, Fadhili Dononda.


Waziri Dk. Mahenge na Meneja wa Biashara wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton Mushi  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Mwandishi Wetu
Makete

Mradi wa ‘SHULE YETU’ unaotekelezwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya AIRTEL umeendelea kunufaisha shule kadhaa nchini kwa sasa umeingia wilayani Makete, Mkoani Njombe na kutoa msaada wa Vitabu vya kiada na ziada vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni 15 kwa shule tano wilayani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk. Binilith Mahenge ndiye aliyepokea shehena ya Vitabu hivyo ambapo pamoja na mambo mengine amesifu Msaada huo kuwa unaunga mkono Juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kufanya mabadiliko makubwa katika sayansi na teknolojia nchini kwa kuwekeza kwenye elimu.

Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo wilayani Makete Mkoani Njombe kwa niaba ya shule zingine zinazofaidika na mradi huo zikiwemo  Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete.

Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Mushi alisema "Kampuni ya Airtel tunakabidhi vitabu vya masomo ya KEMIA, FIZIKIA na HESABU ikiwa ni mwendelezo wa kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha wanafunzi kupenda zaidi masomo ya mchepuo wa sayansi ambapo vyote hivi vinathamani ya shilingi milioni kumi na tano".

Akipokea msaada huo, Dk. Binilith Mahenge ameipongeza Airtel kwa kuungana na Rais Jakaya Kikwete aliyethubutu kufanya mabadiliko kwenye masomo ya sayansi.

Dk. Mahenge alisema "nchi yetu itaendelea endapo tu tutawekeza kwa uhakika katika elimu, mataifa yalioyoendelea leo hii kila kitu kinafanikiwa kuwa kiwango cha elimu cha wananchi wake ni cha hali ya juu".

Kwa upande wao baadhi ya wananfunzi wa shule mwenyeji waliopokea vitabu hivyo kwa niaba ya shule nyingine wameeleza kufurahia kwao kupokea msaada wa vitabu hivyo vitakavyokuwa ni suluhisho la uhaba wa vitabu unavyowakabili wanafunzi wa shule 16 za sekondarii zilizomo wilayani Makete.

"Tunaishukuru sana Airtel sisi wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iwawa tutavitumia kwa uangalifu kwa manufaa ya wengi na pia tunawaahidi Airtel na Mheshimiwa Waziri kuwa tutahakikisha tunapata matokeo ya ufaulu mzuri kwa kuvitumia ipaswavyo" alisema Kiranja mkuu wa Shule hiyo.

Airtel imeanzisha mpango wa Airtel Shule yetu ili kuendeleza Elimu Inchini Tanzania kwa kusaidia shule mbalimbalikali ambapo hadi sasa zaidi ya shule 15000 zimeshapewa vitabu vya kiada kupitia mradi huo.

No comments: