Mratibu wa
Uhurumarathon Innocent Melleck kulia akizungumza na waandishi habari jijini Dar
Es Salaam juu ya Mbio za uhuru kuanzisha mpango wa kuzindua kituo cha michezo
eneo la Msoga linalijulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sport Accademy
ambapo kituo hicho kitagarimu jumla ya shilingi 4.8Bil ambapo kitashirikisha
jumla ya michezo kumi na moja na madarasa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato
cha sita,Kulia ni Katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania Selemani Nyambui.
Xxxxxxxxxxxxx
Na Mwandishi wetu
Wakati usajili kwa watu
wanaotaka kushiriki mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon,
zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam ukiendelea
kwa kasi kubwa waandaaji wa mbio hizo wamezindua mpango wa kujenga kituo cha
michezo eneo la msoga mkoani pwani.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent
Melleck alisema,kamati ya uhurumarathon imeona umuhimu wa kuanzisha kituo hicho
ambapo jumla ya shilingi bilioni nne nukta nane (4.8bl) zinatarajiwa
kutumika katika kukamilisha mpango huo
“Tunapenda kutangaza rasmi
kwamba Uhurumarathon imenunua shamba eneo la msoga mkoani pwani lenye ukubwa wa
ekari ishirini na tano kwa lengo la kujenga kituo kikubwa cha kukuza vipaji vya
wanamichezo mbalimbali mkoani pwani eneo la msoga na kitajulikana kwa jina la
Jakaya Kikwete Uhuru Sports Accademy na jumla ya michezo kumi na moja
itahusishwa katika mkakati huo.
Tunatarajia kumkabidhi
mheshimiwa Rais Kikwete mpango huu wenye lengo la kuleta mafanikio makubwa ya
michezo nchini ambapo watoto wenye vipaji watapata nafasi ya kusoma na kukuzwa
katika utaratibu wa michezo na tunaamini kuwa baada ya miaka mitano hadi kumi tutaweza
kuanza kupata mafanikio.
Kituo hiki ndicho kituo pekee
katika ukanda wan chi za Afrika mashariki na kati ambapo jumla ya wanamichezo
2300 wataweza kuwa katika mpango wa awali.
Tunatarajia kupata nguvu toka
katika wahisani mbalimbali wa ndani nanje ya nchi kwa kuwa wapo wanaohitaji
kuona Tanzania ikipata mafanikio kupitia michezo.
Wakati huo huo Zaidi ya
wakimbiaji 2700 wameshachukua form kwaajili ya kushiriki mbio za mwaka huu huku
malengo makuu yakiwa ni kuhitaji kushirikisha Zaidi ya wakimbiaji elfu kumi na
tano.
Vituo vitakavyokuwa vikiuza
fomu za ushiriki ni 1.Triple seven Mikocheni.2.maduka ya TSN,Uchumi
supermarkets,Uwanja wa Leaderds Club,Ofisi za Rt Taifa,Standi kuu ya mabasi
moshi mjini,Arusha na katika tovuti ya WWW.UHURUMARATHON.COM au kwa kupiga simu 0688108384
No comments:
Post a Comment