Tangazo

December 3, 2014

BENKI YA CRDB YASAINI MKATABA WA HALI BORA ZA WAFANYAKAZI WAKE

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uwekaji saini wa Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga na Katibu wa Benki, John Rugambo. 
 Baadhi ya maofisa wa CRDB wakiwa katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Dorah Ngaliga, Katibu wa Benki, John Rugambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akisaini mkataba wa hali bora za wafanyaka wa benki hiyo na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akisaini mkataba wa hali bora za wafanyaka na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John (wa pili kulia).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kulia) na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John, wakibadilishana hati ya Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi wa benki hiyo na TUICO jijini Dar es Salaam. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) na Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO), Shikunzi John, wakibadilishana hati ya Mkataba wa Hali Bora za Wafanyakazi kati ya Chama hicho na Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.   

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB na imetiliana saini mkataba na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Fedha, Viwanda, Huduma na Biashara (TUICO) wa kuboresha hali bora za wafanyakazi wa benki hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema mafanikio yoyote ya kibiashara hayapatikani kama wafanyakazi ambao ndio wazalishaji hwatakuwa na mazingira yenye maslahi bora na motisha mbalimbali.

Dk. Kimei alisema nia ya CRDB ni kuboresha mahusiano kati ya mwajiri na wafanyakazi, kuboresha mazingiraya utendaji kazi ili kuchochea ufanisi, kurasimisha mahusiano kati ya benki na wafanyakazi kwa kuweka miongozo itakayosaidia kupunguza mifarakano kati ya CRDB na wafanyakazi.

“Mkataba huu ni wa miaka mitatu, utasaidia kuajiri na uthibitishwaji wa wafanyakazi kazini, kushughulikia migogoro ya kikazi, uhamisho wa viongozi wa chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi,utaratibu wa likizo ya uzazi, likizo ya ugonjwa, ulipwaji gharama ya usafirishaji mizigo kwa wafanyakazi wanaohamishwa, mazishi ya wazazi wa wafanyakazi, bima na utoaji tuzo,”alisema  
Aidha alisema.

No comments: