Tangazo

December 16, 2014

JAJI FREDERICK WEREMA AJIUZULU NAFASI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALIMwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (pichani), amejiuzulu wadhifa wake kuanzia hii leo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa leo na Mkurugenzi wake, Salva Rweyemamu kwa vyombo vya habari imethibitisha kujiuzulu kwa Werema kuanzia jana.

Alikuwa kwenye wadhifa huo tangu mwaka 2009 alipochukua nafasi ya Johnson Mwanyika aliyestaafu.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Rais Jakaya Kikwete amekubali ombi la kujiuzulu kwa mwanasheria huyo.

No comments: