Tangazo

December 19, 2014

KIFO CHA AISHA MADINDA CHASOGEZA MBELE ONYESHO LA MIAKA 16 YA LUIZER MBUTU TWANGA PEPETA

Onyesho la kuadhimisha miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta, limeahirishwa kutokana na kifo cha dansa wa zamani wa Twanga Aisha Madinda.
 
Onyesho hilo la aina yake lilikuwa lifanyike Jumamosi hii ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni na lilitarajiwa kushirikisha nyota wengi waliowahi kufanya kazi na Luizer, akiwemo Aisha Madinda.
Mmoja wa wakurugenzi wa Aset inayomiliki Twanga Pepeta, Omar Baraka amesema kutokana uzito wa msiba wa Aisha Madinda na kwa kuzingatia kuwa angekuwa mmoja wa washiriki wa onyesho hilo, wamelazimika kulisogeza mbele.
“Tutawatangazia wadau ni lini onyesho hilo litafanyika, lakini matarajio ni mwezi Januari,” alisema Omar Baraka.
Hata hivyo Twanga Pepeta watafanya onyesho la kawaida Mango Garden kama ilivyo Jumamosi zingine. Source: Saluti5

No comments: