Tangazo

December 19, 2014

UPASUAJI MWILI WA AISHA MADINDA WASHINDIKANA, SASA UTAFANYIKA IJUMAA ASUBUHI …huenda ikabadili muda wa mazishi

Kile kinachoonekana kama aina fulani ya urasimu, upasuaji (postmortem) wa mwili wa dansa Aisha Madinda uliokuwa ufanyike leo mchana (Alhamisi) umeshindikana na sasa utafanyika kesho (Ijumaa) asubuhi.
Meneja wa Aset, Hassan Rehani ameiambia Saluti5 kuwa mwili wa Aisha aliyefariki Jumatano asubuhi ulihamishwa kutoka Mwananyamala Hospitali kwenda Muhimbili kwaajili ya upasuaji ili kujua chanzo cha kifo, lakini ikashindikana kwa madai ya muda wa kufanya upasuaji umekwisha.
Hassan Rehani amesema Muhimbili wamedai mwisho wa kufanya ‘postmortem’ unakwisha saa nne asubuhi na hivyo zoezi hilo sasa litafanyika Ijumaa asubuhi chini ya usimamizi wa polisi.
Kwa hali ilivyo, kama utatokea urasimu au ucheleweshaji wowote wa kuufanyia uchunguzi wa mwili wa Aisha Madinda, basi ni wazi kuwa ratiba ya mazishi inaweza kubadilika.
Aisha Madinda alitarajiwa kuzikwa Kigamboni Ijumaa mchana mara baada ya sala ya Ijumaa. Mwanzoni kabila ilikuwa azikwe Alhamisi saa 10.
Wakati familia ya Aisha Madinda ilikuwa radhi kumzika ndugu yao bila ya uchunguzi zaidi, polisi iligoma kabisa na kusema kwa mazingira ya kifo chake, upasuaji ni suala la lazima. Source Saluti5

No comments: