XXXXXXXXXXXXXXXXXX
· Airtel yaja na Huduma mpya sokoni ya malipo ya
kadi kwa kupitia huduma ya Airtel Money Near Field Communication
(NFC)
· Airtel yalete Huduma ya kulipa kwa kugusisha kadi ya Airtel
Money kwa mara ya kwanza nchini
· Wateja na wafanyabiashara wawezeshwa kufanya miamala kirahisi
zaidi kwa
kugusisha kadi ya Airtel Money
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo (mwishoni mwa wiki) imetangaza huduma ya kwanza sokoni inayotumia kadi maalumu kwa
kupitia huduma ya Airtel Money. Huduma hiyo mpya inayowawezesha wateja wa
Airtel Money kufanya malipo kwa kutumia kadi imeanza katika mkoa wa
Arusha na itaendelea kufikishwa katika mikoa mbalimbali nchini
Akiongea kuhusu huduma hiyo,
Mkurugenzi wa Airtel Money Aijaza Khan alisema” technologia inakuwa kwa kasi na
tumeonelea ni muhimu kwenda sambamba na mabadiliko hayo kwa kuleta huduma za
kibunifu zitakazokithi mahitaji ya wateja wetu yanayokuwa kwa kasi kila siku. Nia
yetu ni kuona wateja wetu wanapata huduma za kisasa kwa wakati wote. Huduma hii
mpya tunayoitambulisha leo itawawezesha wauzaji na wanunuzi kupata njia rahisi,
ya uhakika na salama ya kufanya miamala na malipo yao ya kila siku. ili
kutumia huduma hii kila mteja atatakiwa kupata kadi maalum inayomuwezesha
kufanya malipo kirahisi , kwa haraka na kwa usalama katika maduka mbalimbali
yaliyopatiwa vifaa maalumu kwaajili ya kupokea malipo toka kwa
wateja. Huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wafanyabiashara na wateja wetu
Arusha.
“Kadi hii maalumu imeunganishwa
na akaunti ya Airtel Money ya mteja, mteja anachotakiwa ni kugusisha kadi yake
na kifaa cha kupokea malipo (POS) ili kuweza kufanya malipo. Malipo
yatakamilika pale mteja atakapothibitisha muamala kwa kuweka namba
yake ya siri kwenye kifaa cha malipo
Tunajivunia kuwa mtandao wa
kwanza Tanzania kuanzisha huduma hii ya kibunifu itakayowawezesha wateja wetu
kufanya malipo ya kwa urahisi, haraka , kiusalama bila kuwa na haja ya kupiga
namba ya Airtel money na kuingia kwenye orodha, Kwa kutumia kadi maalumu mteja
anaweza sasa kufanya malipo. ”. aliongeza Khan
Akiongea kuhusu faida za huduma
hiyo , Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” huduma hii inafaida
nyingi kwa wafanyabishara na wateja ikiwa ni pamoja na njia salama ya kuifadhi
pesa, ya kuhakiki na kukusanya pesa,mfanyabiashara anaweza kuzipeleka moja kwa
moja benki kutoka kwenye kifaa hicho au kutoa pesa kwa wakala aliye karibu. Kwa
upande wa wateja faida hizo ni pamoja na kufurahia urahisi, usalama,
uharaka wa kufanya malipo na pia kuepusha wateja kutembea na
pesa nyingi mfukoni ili kufanya malipo. Mteja atakapopoteza au
kuibiwa kadi yake pesa zake kwenye kadi yake zinabaki salama aliongeza” Matinde
Akiongelea kuhusu uzoefu
alioupata a kutumia huduma hii ya kadi kupitia Airtel Money, Mfanyabiashara na
milliki wa Phamarcy Bi Elizabeth Mshana alisema” Huduma hii ni ya kipekee na
imerahisisha sana namna ya kufanya biashara maana ni rahisi kutumia na ni
salama. Wateja wanapokuja dukani kununua dawa na hawana pesa taslimu mfukoni
wanatumia huduma hii na mimi kama muuzaji nafurahi kwakuwa pesa zangu ziko
salama na sina haja ya kufikiri kuhusu kutafuta chenji. Kwa kweli ni huduma
nzuri na tunaifurahia na nawashauri wafanyabiashara wenzangu na
wateja kutumia huduma hii kwani inaleta ufanisi”
Huduma hii inapatikana sehemu
mbalimbali ikiwemo maduka ya biadhaa , maduka ya chakula, maduka ya dawa,
mawakala wa Airtel Money na Baa, Mpango mkakati ni kufikisha huduma hii katika
maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka huu.
Airtel kupitia huduma yake ya
Airtel Money hivi karibuni imezindua huduma nyingine ya kibunifu ijulikanayo
kama Timiza inayowawezesha wateja wake kupata mikopo rahisi papokwa
papo na kurejesha baada ya wiki moja au mwenzi huduma ambayo imewawezesha
watanzania wengi kuboresha mitaji ya biashara zao na kutatua changamoto
ndogondogo za kila siku
No comments:
Post a Comment