Tangazo

January 2, 2015

MWANZA QUEENS WAICHAPA MARA QUEENS GOLI 6 KWA 1 KATIKA MECHI YA UZINDUZI WA WOMEN TAIFA CUP MCHEZO ULIOCHEZWA JIJINI MWANZA

Kikosi cha Timu ya Mara (jezi Nyekundu) wakisalimiana na Marefa wa mchezo huo tayari kwa Mtanange wa Women Taifa Cup kuzinduliwa leo jijini Mwanza kwa Kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Mh Jamal Malinzi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Mara kabla ya Mechi ya Uzinduzi wa mashindano ya Mpira wa Miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Women Taifa Cup kuanza katika dimba la CCM kirumba leo Jijini Mwanza
Baadhi ya Viongozi wa Mpira wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Viongozi wa TFF na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Mechi ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Women Taifa Cup kuanza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
 Kikosi Cha Timu ya Mwanza kikiwa tayari kukabiliana na Timu ya Musoma
 Kikosi cha timu ya Mara 
Mtanange ukiendelea
Gari ya Kurushia Matangazo ya Kampuni ya Azam likiwa tayari kwa kurekodi mchezo wa Uzinduzi wa Mashindano ya Women Taifa Cup yaliyozinduliwa leo katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kuzikutanisha timu za Mara na Mwanza.
 Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mtanange wa Mechi ya uzinduzi kati ya Mara na Mwanza katika mashindano ya Women Taifa Cup yaliyoanza leo katika Uwanja wa CCM Kirumba 
 Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Mwanza wakipeana mawazo mara baada ya mapumziko
Kamera man kutoka kampuni ya Azam TV akiendelea na zoezi ka kurekodi mechi ya Uzinduzi kati ya timu ya Mwanza na Mara katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo. Azam Tv ni moja ya Wadhamini wa Mashindano hayo ya Women Taifa Cup yaliyoanza kutimua vumbi leo katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin Bw Johnson Lukaza ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano ya Women Taifa Cup yaliyoanza leo katika uwanja wa CCM Kirumba kwa kuzikutanisha timu za Mara Queens na Mwanza Queens akiongea na Waandishi wa habari za Michezo mara baada ya mechi ya uzinduzi wa Mashindano hayo ya Women Taifa Cup Kumalizika kwa Mwanza Queen Kuichapa Mara Queens Magoli 6 kwa 1

No comments: