DJ Tee (19) ni kijana mwenye ndoto kubwa katika maisha yake.
Baada ya kuona mahangaiko ya vijana kuelekea kwenye mafanikio, wengi
wakiwa wamemaliza shule na vyuo bila kupata kazi, ameamua kuunda redio
stesheni ghetoni kwake aliyoipa jina la Shujaaz, ili aweze kushea
ideas na vijana wote nchini Tanzania kuhusu mbinu mbalimbali za
kuingiza pesa, kuwapa stori za vijana wanaochakarika katika maisha yao
pamoja na kuwaburudisha.
"Nimeamua kuiita Shujaaz
kwa sababu, naamini kuwa kijana ambaye anajituma na kuweka mfano bora
kwenye jamii ni shujaa". Alisema DJ Tee. "Ndoto zangu zinakaribia kuwa
kweli".
Story ya kijana huyu inapatikana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kupitia kijarida cha Shujaaz, kitakachokuwa kinasambazwa kupitia gazeti la Mwanaspoti, kuanzia JUMAMOSI HII
ya tarehe 28. Kwenye kijarida hicho, utapata ideas mbali mbali ambazo
vijana wanaweza kuzifuata na kujiingizia kipato. Pia, kutakuwa na stori
za vijana wengine kama Pendo, Semeni na Pepe ambao ni mashabiki wakubwa
wa DJ Tee na redio show yake ya Shujaaz.
Kijana huyu ameamua kujiita DJ Tee
ili asijulikane na watu wake wa karibu, kwa kuwa ana-hack airwaves za
redio stesheni ili aweze kusikika. Sikiliza redio stesheni uipendayo
kuanzia wiki ijayo, huwezi jua, inawezekana DJ Tee akawa hewani!
Wewe pia USIKOSE kuwa sehemu ya mafanikio na harakati za kijana huyu kwa kujiunga naye. Pata nakala yako ya Shujaaz kuanzia Jumamosi hii (28/02/2015) kupitia gazeti la Mwanaspoti. Pia, jiunge naye kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa jina DJTee255 ili upige naye story na wewe uweze kushea idea zako za hustle. Unaweza pia ukampata Instagram na Twitter kwa jina @djtee255
No comments:
Post a Comment