![]() |
Sehemu za Nyumba zilizoathiliwa na
Mafuriko hayo.
|
![]() |
Mmoja wa waathirika wa Mafuriko huko
Kahama, Bi. Helen Benjamin akiongea juu ya hali halisi ya maafa hayo na kuomba
serikali kuwapatia msaada.
|
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo
imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika wilaya ya kahama mkoani shinyanga
kwa kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu yanayoitajika kwa sasa. Zaidi ya watu
35 walifariki na kuwaacha mamia wakiwa hawana makazi ya kukaa kufatia mvua
kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu.
Akionge wakati wa makabithiano ya msaada
huu, Meneja mauzo wa Airtel Shinyanga Bwana Ezekiel Nungwi alisema” Tunaungana
kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizopoteza marafiki na
wanafamilia kutokana na mafuriko haya.
Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha
wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo
tunaungana kwa pamoja kutoa msaada kwa namna tutakayoweza .
Leo kwa niaba ya
Ofisi yetu ya kanda ya Shinyanga tunatoa msaada wa mabati, mablanketi, magodoro
pamoja na chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 3 na kuwaomba watanzania
kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa kahama ili kuepuka milipuko ya magonjwa
isitokee na kuwawezesha kurudi kufanya shughuli zao za kawaida mapema
iwezekanavyo.
Sambamba na mchango huu, tunapenda
kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watanzania kuchangia. Tunachukua fulsa
hii kuwaomba wateja wetu kuchangia kwa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA kwenda
namba 15626 , ujumbe huu utalipiwa shiling 256 na pesa hiyo itaingia kwenye mfuko
wa kuchangia wahanga wa mafuriko mkoani Shinyanga.
Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kahama
helen Benjamin Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu ulikuja wakati
tunauhitaji zaidi, Tunawashukuru kwa kuanzisha namba itakayowapa fulsa
watanzania kuchangia, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchagia na kwa
makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka
kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli
zetu za kiuchumi zimeteketea.
Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba
muendelea na moyo huo wa kujitolea.
No comments:
Post a Comment