Tangazo

August 1, 2012

Mzee Mwinyi kuongoza harambee ya Islamic Help ya kuchangia yatima wa Kisemvule Agosti 03, Serena Hotel

Afisa Programu wa Asasi ya Islamic Help, Adam Rajab (wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu hafla ya Futari na chakula cha usiku iliyoandaliwa na Asasi hiyo Ijumaa Agosti 3.2012 katika Hoteli ya Serena, kwa ajili ya kuchangisha fedha za ujenzi wa nyumba katika kijiji cha watoto yatima 'Childrens Eco Village' huko Kisemvule ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kushoto ni Afisa Utawala wa Islamic Help, Saamia Shikely (Kutoka wa tatu kushoto) ni; Meneja wa Islamic Help Tanzania, Ishak Muhsin, Mwanachama Mshauri wa Bodi, Salehe Ally na Mkurugenzi wa Vision Investment, Ally Nchahaga. Picha na Daily Mitikasi Blog
******************
Nasaidia ili kuleta mabadiliko'  ‘ unasikika mwito wa kushiriki katika futari na chakula cha jioni kilichoandaliwa na Asasi ya  Islamic Help Tanzania ili kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa  ‘ Children’s eco village’ huko Kisemvule, Dar es salaam.
Hafla hiyo itafanyika tarehe 3 Agosti  2012 kuanzia saa 12.00 jioni katika Hoteli ya Serena jijini  Dar es Salaam. Rais mstaafu Mheshimiwa  Ali Hassan Mwinyi, atakuwa mgeni rasmi ambapo Kiasi cha zaidi ya wageni 400, wakiwemo wahisani na wakereketwa wengine wanatarajiwa kuhudhuria katika hafla hiyo .
Makazi ya watoto ya The Children’s Eco village yana jumla ya nyumba  16 kwa ajili ya watoto yatima  160.

Makazi hayo yako katika eneo la ekari 30 lenye uoto mwanana wa kijani na hali nzuri ya tabia nchi Ni katika eneo hilo la kuvutia ndiko ambako mradi unatarajia kujenga makazi rafiki kimazingira yaliyosheheni vionjo vyote vya vivutio vya kisasa.

Ujenzi  unakusudiwa kuzingatia kwa kiwango cha hali ya juu matumizi madogo ya nishati pamoja na ya ardhi . Aidha mradi unatarajiwa kutumia teknolojia ya nishati rafiki kwa mazingira, mbinu nzuri za usimamizi wa utupaji taka, na teknolojia ya urejelezaji.

Matumizi ya ardhi yaliyo rafiki kwa mazingira pamoja na yabiogesi yatakuwa ni uhakikisho wa  kuweko  kwa mazingira salama na yenye tija kwa shughuli za uzalishaji.

 Kituo cha mafunzo pamoja na shamba vitaanzishwa  kwa awamu kama shughuli za kuingiza kipato kwa kijiji cha makazi ya watoto  pamoja na kuwa  mfano wa ujenzi wa maendeleo ya jamii na wa uwezo  kwa vijiji vya jirani.

Islamic Help
Islamic Help ni Asasi ya misaada  isiyo ya kiserikali (ASIZE) iliyoandikishwa huko  UK . Asasi hii imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ya kiutu kwa zaidi ya nchi ishirini. Kama shirika la maendeleo linaloinukia, hivi karibuni tulishinda  tuzo ya  Oscar ya filamu fupi bora iliyojulikana kama ‘ Saving face’ on Acid burn victims. Tumekuwa tukifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2008 , hasahasa tumekuwa katika kisiwa cha  Mafia  tukijihusisha na  programu ya ukusanyaji fedha kwa  kujitolea, uhamasishaji na ufikiaji.

Progarmu hiyo ambayo imekuwa ikifahamika kama  ‘ Mission to Mafia’ imefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 600 kutoka kwa zaidi ya vijana  55 wa UK na kutekeleza miradi  ya maji, afya, malezi ya yatima na shughuli nyingine. Aidha tangu tufungue ofisi zetu jijini Dar es Salaam tumefanikiwa kutekeleza miradi iliyogharibu zaidi ya shilingi milioni 950.
 
Kwa taarifa zaidi kuhusu  Islamic Help na mradi yake, tafadhali tembelea tovuti yetu ifuatayo www.islamichelp.co.tz au piga simu Namba 0787 487333, kwa Afisa mawasilino wetu  Nadhir Bahyan  au tuma baura pepe kwa anuani: nadhir@islamichelp.co.tz 

No comments: