Tangazo

March 6, 2015

WANAKIJIJI CHA OLOLOSOKWAN -NGORONGORO WAISHUKURU AIRTEL KWA KUWAFIKISHIA MAWASILIANO

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro (kutoka kulia), Diwani wa kata hiyo, Yannick Ndoinyo, Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili Naing’isa, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa UNESCO, Al-Amin Yusuph (wa pili kulia), aliyeongozana na baadhi ya viongozi wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, walipomtembelea ofisini kwake katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutoa shukrani zao baada ya kampuni hiyo kufunga mnara katika eneo lao na kupelekea urahisi wa mawasiliano ikilinganishwa na hapo awali.  Wengine ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi (wa tatu kulia) na Mjumbe wa Baraza la kijiji hicho, Norkishili Naing’isa.

Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Wananchi wa kijiji cha Loliondo mkoani Arusha wametembelea ofisi za Airtel Tanzania jana kwa lengo la kuonana na mkuu wa kampuni hiyo ili kumshukuru yeye pamoja na kampuni yake kwa kuinusuru jamii ya kijiji hicho na changamoto mbalimbali za kijamii, kiuchumi mara baada ya kuwezesha vijiji vyao kuwa na mawasiliano ya mtandao wa simu pamoja na kufungua kituo cha redio ya jamii cha Loliondo.

Airtel ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO walizindua Radio ya jamii katika kijiji cha Ololosokwani Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha mwaka jana na kuhudhuriwa na Waziri wa mawasiliano sayansi na technologia Mh Makame Mbarawa kwa lengo la kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu, elimu duni, ukeketwaji, ukandamizaji wa wanawake na watoto na changamoto zinginezo.

Viongozi wa Kijiji cha loliondo wakiongozwa na diwani Diwani wa Kata ya Ololosokwan, wilaya ya Ngorongoro, Yannick Ndoinyo walikishukuru sana Airtel huku wakiimba kampuni hiyo kuendelea kushirikiana na vijiji vingine kama ilivyofanya kwao kwani sasa imerahisisha mambo mengi ya kijamii na uchumi.

“Tunawashuru Airtel, Mnara mlioweka pale Ololosokwani sasa unasaidia kurahisisha mawasiliano ya simu na pia huduma za kifedha kwa kuwa benki ziko mbali hivyo sasa tunaitumia huduma ya Airtel Money kutuma na kutoa pesa pale kijijini” alisema Bw, Yannick

Pia kwa ushirikiano mlioufanya na UNESCO na katufungulia kituo cha redio ya kijamii kinamafanikio makubwa sana, kimekuwa kikielimisha jamii, kuburudisha na kufahamishana mambo ya msingi anayoendelea nchini.

Kwa upande wake Mkurungezi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “Airtel  tumefanya hili ili kutimiza  jukumu la kusaidia jamii,
Tayari redio Ololosokwani FM, FADECO FM Karagwe, na Uvinza FM Kigoma zimekamilika,  tunajisikia fahari sana kuona mmekuja kutoa neno la shukrani, hii inatutia faraja nasisi kuendelea kusaidia jamii nyingine zenye changamoto zinazofanana na hizi za Ololosokwani.

“Sasa Wakazi wa ololosokwani na vijiji vingine jirani takribani 14 wanajivunia kutangaza utamaduni wao, kuboresha au kupata uongozi bora, kutangaza mazao yao ya  biashara kukuza soko kutumia huduma ya Airtel money kufanya malipo na kuhifadhi pesa zao kwa usalama zaidi,” alisema Colaso.

Pia sasa tutajadiliana kwa pamoja kuiboresha Multimedia center
tuliyoijenga kwa kuiongezea mtandao wetu wa intaneti wenye spidi wa 3.75G, Aliongeza Bw Colaso.

Airtel na UNESCO umedumu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ambapo kumekuwa na mafanikio lukuki kwa kuweza kuzihudumia jamii mbalimbali kupitia mradi wao wa radio za jamii kwa  baadhi ya maeneo kama Sengerema Mwanza,  Chake Chake Pemba, akunduchi Unguja , Pangani Tanga,  Kyela Mbeya , na KaHama Shinyanga yakiwa tayari yanaendesha redio za jamii zikiwa kwenye ufunguzi wa awali wa majaribio (soft
launch).

No comments: