Tangazo

April 11, 2015

Airtel na Benki ya NMB wazindua huduma ya kifedha kwa njia ya mtandao

 Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benk ya NMB, Tom Borgjols wakiwa wameshika bango linaloashilia uzinduzi wa huduma ya kifedha kwa njia ya mtandao kati ya Airtel na NMB, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.


Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia), akipata ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia), kabla  ya uzinduzi wa huduma ya kifedha kwa njia ya mtandao kati ya Airtel na NMB, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benk ya NMB, Tom Borgjols.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx

Dar es Salaam 

Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania wamezindua huduma ya kuweka na kutuma pesa kutoka kwenye akaunti za NMB kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money kupitia simu za mkononi.

Huduma hiyo ya kibunifu itawawezesha wateja kufanya miamala ya kifedha kirahisi, kwa njia salama kupitia simu zao za mkononi na kuboresha huduma za kifedha wakati wowote, popote pale walipo. Lengo kubwa la huduma hii ni kuwezesha huduma za kibenki kuwafikia wateja kwa ukaribu na urahisi zaidi popote pale walipo.

Huduma hii imezinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba katika hoteli ya Serena Jiji Dar es Salaam. Mhe Mwigulu alisisitiza kuwa huduma za fedha kupitia simu za mkononi ni muhimu katika kuililetea Taifa maendeleo.

Mhe.Mwigulu alisema ushirikiano huu ni wa muhimu na serikali inauunga mkono maana umeleta mageuzi katika maisha ya wananchi wa Tanzania pamoja na maendeleo kwa ujumla.

“Ningependa kuishukuru benki ya NMB pamoja na kampuni ya simu ya Airtel kwa kwa kuingia katika ushirikiano huu uliosubiriwa kwa kipindi kirefu na wanachi kati ya kampuni hii kubwa ya simu nchini Airtel na benki inaoyongoza kuwa na mtandao mkubwa wa matawi na mashine za ATM Nchini NMB ambao utatoa nafasi itakayokuza huduma za kifedha nchini Tanzania’ Alisema Mhe. Mwiguli.

Hata hivyo Mhe Mwigulu aliongeza kuwa ukuaji wa uchumi nchini umewasukuma watanzania kutumia  simu zao za mkononi kupata taarifa kuhusu akaunti zao za benki popote pale walipo na kwa wakati wowote hii inainua uchumi wa nchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Airtel Bw.Sunil Colaso alisema, umoja huu ni ishara ya mageuzi katika matumizi ya tekinolojia katika kuboresha maisha ya watanzani kupitia simu za mikononi.

Kwa njia hii, wateja wa Airtel na NMB kwa pamoja wanaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money kwenda kwenye akaunti zao za NMB. Vilevile, mteja anaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda kwenye akaunti ya Airtel Money kupitia simu zao za mkononi. Watanzania hasa waishio vijijini sasa wanaweza kupata huduma za kifedha kwa urahisi pamoja na kuendesha biashara zao kwa kutumia simu zao za mkononi wakati wote.

Bw.Colaso aliongeza kwa kusema kuwa “Tumejikita katika kuendele kuboresha hudumazetu ili kukidhi matakwa ya wateja wetu na tunaamini kupitia mishikamano hii kampuni ya Airtel itazidi  kutoa huduma sahihi na bora kwa wateja na kuwawezesha kukabiliana na changamoto wanazo kumbana nazo kila siku.

Kwa upande wa NMB, Kaimu Mtendaji Mkuu Bw.Tom Borgjols alisema uzinduzi wa huduma ya Airtel Money kwa huduma ya simu ya NMB mobile ni rahisi kwani itawawezesha watu wasio kuwa na akaunti na ambayo hawajatimiza vigezo vya kufungua akaunti wenyewe kupata huduma za kifedha karibu yao.

Bw.Tom aliongeza kuwa “Uzinduzi wa huduma hii ilioungalishwa na NMB mobile itawawezesha wateja wetu zaidi ya 1,000,000 waliojiunga na huduma ya NMB mobile kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money kwenda kwenye akaunti zao za NMB. Vilevile, mteja anaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda kwenye akaunti ya Airtel Money kupitia simu zao za mkononi kwa bei nafuu.

Zaidi wateja wetu wataendelea kufurahia huduma zingine kama, kuweka na kutoa fedha, kulipia bili mbali mbali na kuangalia salio.

Benki ya NMB itatumia mawakala wa Airtel Money na mtandao wao utakaowakeka karibu zaidi na wateja wake kwa  kutoa huduma za kifedha kupitia mawakala wa Airtel Money karibu na makazi yao.

No comments: