Tangazo

April 12, 2015

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL 69 ZA UJENZI WA VISIMA VYA MAJI VITUKA,MWEMBELADU WILAYANI TEMEKE

 Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (kulia), akikabidhi mfano wa hundi ya sh Milioni 69 kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vituka, Bi. Amina Rashid Simba kwa ajili ya kuchimba visima vya maji katika maeneo ya Vituka na Mwembeladu, Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam jana. Wengine katika picha ni Katibu wa Diwani Bw. Ismail Ng'ombo (wa pili kulia), Bw. Kassimu Makoa na Bi. Zubeda Ali Ligubike aliyetoa eneo la mradi huo. (Na Mpigapicha Wetu)
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vituka, Bi. Amina Simba (kulia), akikabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 69 kwa Mhandisi Mo Resources Ltd Bw. Onesmo Sigala zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya mradi wa maji katika mitaa ya Vituka na Mwembeladu, Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TBL, Bi. Doris Malulu, Katibu wa Diwani Bw. Ismail Ng'ombo (wa pili kulia), Bw. Kassimu Makoa na Bi. Zubeda Ali Ligubike aliyetoa kiwanja cha mradi huo. (Na Mpigapicha Wetu)
 Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akimpongeza Bi. Zubeda Ligubike kwa kutoa kiwanja kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji.
 Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akizungumza na wakazi wa Mitaa ya Vituka na Mwembeladu, Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam baada ya kukabidhi mfano wa Hundi ya sh. milioni 69 zilizotolewa na TBL kwa ajili ya mradi wa maji.

 Malulu akikagua mitambo ya kuchimba kisima

No comments: