Tangazo

April 8, 2015

Ally Chocky na Super Nyamwela warejea nyumbani Twanga Pepeta

Kiongozi wa Twanga Pepeta, luixa Mbutu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo. Kulia ni Choki na (kushoto), ni Super Nyamwela. PICHA/HISANI YA SALUTI5

 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Daily Mitikasi Blog
Dar es Salaam

Mwanamuziki wa dansi mkongwe nchini, Ally Chocky amejiunga rasmi na African Stars wana Twanga Pepeta.

Chocky alitangazwa leo na uongozi wa Twanga Pepeta katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Nemax iliyopo Kinondoni jijini  Dar es Salaam.

Aidha Chocky amejiunga pamoja na mcheza shoo mkongwe Super Nyamwela.

Onyesho la kwanza la Chocky katika bendi hiyo litakuwa tarehe 18 mwezi huu, katika ukumbi ambao utatangazwa baadae.

“Tayari nna tungo tatu nitakazoanza nazo ambazo ni ‘Usiyaogope maisha’, ‘Kichwa chini’ na ‘No discussion’, alibainisha Chocky katika mkutano huo.

Mkutano huo pia ulihudhuliwa na Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka na Kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu.

No comments: