Tangazo

April 19, 2015

Mtanzania Nalimi Mayunga aibuka mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kumtangaza mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Mayunga Nalimi (katikati), katika tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia), ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akimkabidhi tuzo mwimbaji Mayunga Nalimi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, katika tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia), ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza (kushoto), akimpongeza mwimbaji Mayunga Nalimi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, katika tafrija iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (kulia), ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Dar es Salaam

Mwakilishi kutoka Tanzania katika shindano la Airtel Trace Music Star Afrika Nalimi Mayunga  ameibuka mshindi na kuwacha hoi washiriki wengine kutoka nchi 13 barani Afrika  waliokuwa wakishindania kinyanganyiro hicho  katika mashindano ya fainali za Afrika yaliyofanyika Naivaisha Kenya

Akimtangaza  mshindi mwanamuziki nguli kutoka Marekani na jaji katika shindano hilo Akon alisema” Nimefurahisha sana na Mwanamuziki huyu chipukizi kutoka Tanzania kwani anao sauti nzuri iliyotulia na uwezo mkubwa wa kuiba. Mayunga ananikumbusha enzi zangu, na naamini akiendelea hivi na kupata mfunzo zaidi atafika mbali katika tasnia ya muziki. Naahidi kumpa mafunzo yatakayomsaidia kupata mbinu mbalimbali za kimuziki na kurekodi nyimbo nae moja,  lakini akifanya vizuri nitampa zawadi ya kurekodi album pamoja nami”.

Akiongea katika halfa ya kumtangaza mshindi iliyofanyika high spirit, IT plaza jijini Dar es saalam  Mkurugenzi wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” Shindano la Airtel Trace Music Star lilizinduliwa Oktoba mwaka jana,  lengo likiwa ni  kusaka, kukuza vipaji vya muziki na kuwawezesha wanamuziki chipukizi wa kitanzania na Afrika kujulikana katika anga za muziki duniani. 

Leo tunayofuraha kutimiza dhamira yetu kwa vitendo  kwa kuwaweezesha watanzania kupata nafasi ya kushiriki na hatimaye moja kati yao kushinda.  Nampongeza sana Nalimi Mayunga kwa ushindi huu na tunaamini nafasi hii ya kupata mafunzo na kurekodi na Akon utakuwa mwanzo wa safari yake ndefu ya mafanikio na kuzifika ndoto zake”.

“Airtel tunajisikia furaha kuwa sehemu ya mafaniko ya vijana wengi kuzifikia ndoto zao kupitia program zetu mbalimbali ikiwemo hii ya Airtel Trace Music Stars. Tunaahidi kuendelea kuwapatia fulsa watanzania kupitia program zetu mbalimbali za kijamii huku tukiendelea kutoa huduma bora na za kibunifu na kuwafikishia watanzania mawasiliano bora nchini.” Aliongeza Colaso

Kwa upande Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mungereza alisema “ Nachukua fulsa hii kumpongeza sana Mwakilishi wetu Nalimi Mayunga kwa kupeperusha vyema bendera ya nchi yetu na kurudi na ushindi.

Nimefatilia mshindano haya yalikuwa ni na ushindani mkubwa sana, hii inaonyesha ni jinsi gani Tanzania tulivyo na vijana wenye vipaji lakini hawajapata nafasi ya kuvionyesha, nawapongeza sana Airtel kwa kuja na mashindano haya yanayowawezesha vijana wa kitanzania kupata fulsa ya kuonyesha uwezo wao na kufanikiwa zaidi.

Sisi kama Baraza lenye dhamana ya kusimamima sanaa nchini tumefurahia sana program hii na tunajivunia  ushindi huu mkubwa kwa nchi yetu na tunamtakia kila laheri mayunga na  tunaamini ataendelea kufanya vizuri katika safari yake ya muziki pindi atakapoenda nchini marekani kupata
mafunzo zaidi na kurekodi nyimbo yake na Akon.

Akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi mayunga alisema “ najisikia furaha sana , kwakweli na mshukuru Mungu sana kwani ushindani ulikuwa mkali sana lakini nashukuru niliweza kukabiliana nao kwa kufata maelekezo ya walimu ya kupumzisha sauti na kufata mbinu za kimuziki wakati wa kuimba na kuwa na ujasiri. Nimefurahi sana kwa vile nafasi hii niliyoipata kupitia ushindi huu ni kubwa na yakipekee. 

Nawashukuru sana Airtel kwa kuanzisha mashindano  haya na nawahaidi watanzania kufanya vizuri zaidi na kuendelea kuipeperusha bendera ya nchi yetu sehemu mbalimbali ntakazokwenda katika shughuli zangu za kimuziki.

Mashindano hayo yalishirikisha washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda , Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Congo (DRC), Gabon na Tanzania  huku yakisimamiwa na majaji mahiri akiwemo  Akon, Devyne Stephens na Lynnsha .

Washiriki hao 13 walichujwa na kupatikana 6 bora ambao ni wawakilishi toka Uganda, Madagscar, Malawi, Tanzania, Nigeria na Congo Brazaville , washiriki hao waliimba Acapella  ili kuonyesha uwezo wa sauti zao ambapo  Tanzania, Nigeria na Congo B  walifudhu kuingia tatu bora mwakilishi kutoka Tanzania aliibuka mshindi  akifatiwa na mshiriki toka Nigeria na mshindi wa watatu ni mwakilishi kutoka Congo Brazaville,  mbali na kukabithiwa milioni 50 baada ya kuibuka mshindi hapa Tanzania, Mayunga amepata deal la kuredo na kupata mafunzo nchini Marekani vyenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500,000.

No comments: