Tangazo

April 19, 2015

Balozi Henry Mdimu wa Imetosha Foundation atoa wito kwa vyombo vya habari na jamii!


Balozi Henry Mdimu akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi mjini Mwanza.


Henry Mdimu ametoa wito kwa vyombo vya habari na jamii nchini kulichukua suala la ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino kama lao ili kuiondoa nchi yetu katika aibu hii. Aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi ambao ni wadhamini wa habari wa ujio wa kamati ya Imetosha katika kanda ya ziwa.
Kutoka kushoto ni Salome Gregory, Henry Mdimu Mgaya, Issaya Mwakilasa na Zaytun Biboze.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Balozi Mdimu

Imetosha
Kila sauti inasikika.
PIGA KELELE uunge mkono haki ya KUISHI

Ndugu waandishi wa habari, Mwakilishi wa Tanzania Bloggers Network, mabibi na mabwana…..

Tuko hapa kuueleza Ulimwengu kupitia vyombo mbali mbali vya habari juu ya harakati yetu ya IMETOSHA. Harakati hii hii  imeanzishwa na mimi mwenyewe, Henry Mdimu, mwanahabari mwenzenu ambaye nimeamua kwa moyo mmoja kuwa Balozi wa kujitolea wa harakati za kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu  wa ngozi, maarufu kwa jina la Albino.

Mimi na ujumbe wangu tumekuja Mwanza kutambulisha harakati za IMETOSHA na ikiwa sehemu ya kuandaa shughuli zitakazofanyika kanda ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kupambana na mauaji na unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Mwezi ujao ujumbe wa IMETOSHA utakuja na kuweka kambi ya kudumu Mwanza itakayozunguka kanda ya Ziwa na kutembelea nyumba kwa nyumba zenye wahanga wa matukio ya mauaji na kutoa elimu kwa jamii kuwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hayasababishi utajiri.

Pamoja na shughuli tutakazofanya tukiwa Kanda ya Ziwa mwezi wa tano ni pamoja na maetmbezi ya hisani, kutakua na mpira kati ya Simba na Yanga ambapo IMETOSH itavalisha wachezaji Thisrts zake ikiwa ni sehemu ya kutangaza harakati zetu.


Pia tutakua na tamasha litakaloshirikisha wasanii mbalimbali watakaotumbuiza nyimbo mbamimbali zitakazokua na ujumbe wa kukemea na kupinga mauaji na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.


Nimeamua kufanya hivi baada ya kushuhudia ndugu zangu wakiteseka kwa muda mrefu. Awali nilishindwa kuanzisha harakati hizi nikiamini kuna vyombo vinavyohusika na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Hrakati hizi zimeanza baada ya kuona kadri muda unavyokwenda matukio yamezidi kuongezeka na hali kuwa mbaya. Nashuhudia ndugu zangu wakinyanyaswa, wakibezwa mtaanai na hata kudhihakiwa huku baadhi ya wanaoshuhudia haya wakicheka tu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na vyombo vya habari vilimkariri Rasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania muheshimwa Jakaya Kikwete akisema kesi mbili za mauaji ya watu wenye ulemavuwa ngozi zililipotiwa kwa mwaka 2012 na 2013.

Taarifa hizo ziliongeza kuwa kti ya mwaka 2006 na 2015, watuhumiwa 139 wameshikiliwa na kesi 35 zimeandikishwa. Watuhumiwa 73 waliachiwa huru na wengine 15 wamekutwa na makosa. 

Hivyo nimeamua niweke jitihada zangu binafsi niisaidie Serikali yangu katika kuondoa doa hili linaloichafua Nchi  yetu yenye sifa ya Amani duninia nzima. Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu mniunge mkono tukishirikiana na Serikali ili mauaji haya yakome.
Kutokana na ushawishi nilionao kama Mwandishi, Mtangazaji wa redio na Blogger naamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki ya kusihi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki historia. Salamu zangu ziwafikie wanyanyasaji, wauaji na wenye kufanya dhihaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuwa IMETOSHA.

Uchunguzi wangu wa awali umebaini ukosefu wa elimu juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi hupelekea tatizo hili kukua na hatimaye kuuana kw aimani za kishirikina. Hivyo basi, silaha ya Elimu ni sehemu kubwa ya haraki hizi.

Mimi pamoja na mafariki zangu wanaoniunga mkono tutakwenda Kanda ya Ziwa kutoa Elimu kabla tatizo hili halijaenea Nchi nzima. Swali moja tujiulize kwa nini Kanda ya Ziwa? Tutatoa Elimu kwa njia ya ushauri nasaha, pia wanamuziki  sanaa.

Nina mpango wa kwenda kanda ya Ziwa kuhangaika na hili mpaka nione mwisho wake. Na ni rahisi kumaliza hili tatizo kabla halijaenea nchi nzima. Maana Walemavu wa ngozi wako nchi nzima lakini jiulize kwa nini Kanda ya Ziwa tu?

Mimi pamoja na rafiki zangu hawa, tunatoka kuelekea huko kutoa elimu kwa njia ya sanaa, na washauri nasaha. Pia tutakua na team ya wanamuziki wanaoandaa nyimbo mbali mbali za kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili huu.

Wasanii hao ni paoma na Jhikoman, Kassim Mganga, Profesa J, Ray C, Fid Q, Roma Mkatoliki na Dami Msimamo.  Tutaishi na jamii hii kwa muda tukiongea nao kwa lugha yao kwa kutumia wakalimani kwa wsifahamu Kiswahili kuwashawishi waamini hakuna ukweli katika Imani hizo.

Naamini nguvu ya vyombo vya Habari hivyo naomba ushirikaiano wenu katika kuhakikisha tunatokomeza mauaji ya wenzetu ili mwisho wa siku wanunuzi wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi wafukuzwe watakaanza kuuliza jinsi ya kufanya mauaji haya.
Harakati za IMETOSHA rasmi zimezinduliwa rasmi tarehe 3/3/2015.

Mungu atubariki. 

Ahsanteni
HENRY MDIMU-0715000881 na 0787000880
Balozi wa kujitolea
Harakati za IMETOSHA

SALOME GREGORY 0717367309

Mratibu wa Habari- Harakati za IMETOSHA

No comments: