Tangazo

April 16, 2015

TANZIA: CHE MUNDUGWAO AFARIKI DUNIAMwanamuziki Mkongwe wa Nyimbo za Asili hapa nchini, Joseph Chigwele Che Mundugwao (pichani) amefariki Dunia mapema leo asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es salaam.

Kabla ya kufikwa na mauti, Che Mundugwao aliugua na kulazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa muda mrefu. 

Che Mundugwao alikuwa anashikiliwa katika gereza la Segerea kwa kukosa dhamana ya kesi yake, ya kukutwa na pasi za kusafiria 12 za watu tofauti tofauti bila kuwa na maelezo yake.

Marehemu Chigwele Che Mundugwao amewahi kulipatia taifa sifa kimataifa katika nchi za Scandinavia ambako alijipatia mialiko mbalimbali ya kuwaburudisha mashabiki wake wa muziki.

Miongoni mwa bendi ambazo amewahi kuimbia ni pamoja na Tatu Nane.

Marehemu Che Mundugwao aliyezaliwa mwaka 1968 amefariki akiwa na umri wa miaka 47.

No comments: