Na Magreth
Kinabo
Tume Taifa ya Uchaguzi(NEC) imeongeza siku nne zaidi
kwa mkoa wa jiji la Dar es Salam kujiandikisha
katika daftari la kudumu la kupiga
kura ili kuwezesha wakazi wengi kujiandikisha.
Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini
Dares Salaam Mwenyekiti wa tume hiyo
Jaji Mstaafu Damian Lubuva (pichani), alisema uamuzi huo umetokana na kuwepo kwa
mwamko mkubwa wa wananchi
waliojitokeza kwa wingi isivyo kawaida katika vituo mbalimbali.
“Tume
imeamua kuongeza musa wa kulizia watu watakaokuwapo vituoni siku ya mwisho
yaani kesho tarehe 31,Julai, mwaka 2015. Sasa
muda umeongezwakwa siku nne ili kumalizi unadikishaji huo,|” alisema
Jaji Lubuva.
Jaji
aliongeza kwamba hivi sasa hadi kufikia jana tarehe 29, Julai wananchi
waliojiandikisha katika daftari hilo ni
18,826,718 kwa nchi nzima , wakati lengo lilikuwa ni kufikia wananchi milioni
23 hadi 24.
Alisema hadi
siku ya jana watu waliojiandikisha katika jiji hilo ni 1,754,725 sawa na asiliamia 62.4,wakati makadrio ni watu 2,810,423.
No comments:
Post a Comment