Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said
Magalula (kulia), akiwa na Mkurugenzi
wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba baada ya mkuu huyo,
kuzindua Duka jipya la Airtel Tanzania lililopo katika Barabara ya Uhuru jijini
Tanga jana.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua duka lake jipya katika mkoa
wa Tanga ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha inawapatia wateja wake nchi
nzima huduma bora na za kisasa.
Duka hilo la
kisasa, liko katika maeneo ya tanga mjini, Barabara ya Uhuru, kwenye
jingo la nyumbani hoteli. Huduma zinazotolewa na duka hilo ni pamoja na
kukusanya Ankara, kurudisha namba zilizopotea, mauzo ya simu hasa smartphone,
Airtel money, kusajili namba pamoja na huduma za kimitandao.
Akiongea wakati wa
uzinduzi , Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa Airtel, bi Adriana
Lyamba alisema” uzinduzi wa duka hili ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma bora na kuwapatia wateja wetu uzoefu toufati katika huduma zetu. Leo tunawawezesha wateja wetu na wakazi wa mkoa wa Tanga kupata hudumu muhimu kama vile za kifedha za Airtel Money kwa usalama zaidi pamoja na kuwaunganisha na simu za kisasa za smartphone na huduma zetu za intaneti”.
“Sambamba na hilo,
duka letu pia litatoa ofa kabambe za simu na vifaa vya aina tofauti na kuwawezesha wateja wetu kunganishwa na tecknologia ya simu za mkononi ya kisasa Tunaamini vifaa vya kisasa ni sehemu muhimu ya
mahitaji ya wateja wetu kwa sasa, hivyo kupitia watoa huduma wetu
waliobobea kwenye maswala ya tekinologia tunawewezesha wateja wetu kuchangua
vifaa na simu bora pamoja na kuwaunganisha na huduma za intanet. Ni matumanini
yangu kuwa wateja wetu sasa watapata suluhisho la mahitaji yao ya huduma za
simu kwa urahisi kupitia duka hili.” Aliongeza Lyamba.
Akizindua duka hilo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Magalula Said Magalula alisema “Mawasiliano yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuwaunganisha watu na
biashara na kukuza uchumi wa nchi. Nawapongeza Airtel kwa kuongeza wigo kupitia
huduma kwa wateja na kuleta mabadiliko ya kibunifu. Tunaamini ubunifu huu
utawawezesha wakazi waTanga kupata huduma bora wakati wote, na kwa hilo
Tunawashukuru sana Airtel.
“Natoa wito kwa wakazi
wa Tanga na wateja wa Airtel kutembelea duka hili na kufurahia huduma na bidhaa za kisasa ikiwemo huduma ya Airtel Money inayotoa suluhisho kwa mahitaji yao ya huduma za kifedha, kufanya malipo na kutuma pesa kirahisi zaidi” alisema Magalula.
Mkuu wa Mkoa aliwaasa
makampuni mengi zaidi kuiga mfano wa Airtel katika kutoa huduma bora na kusema Serikali iko tayari kushirikiana nao katika
kuhakikisha inaboresha maisha ya wakazi na watanzania wa ujumla katika maeneo
mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment