Tangazo

July 30, 2015

LOWASSA ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS CHADEMA

Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Edward Lowassa, (kulia), akionyesha mkoba wenye fomu za kuomba kuwania urais kupitia CHADEMA, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mh. Freeman Mbowe, kwenye makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2015. Mh Lowassa, alijiunga hivi karibuni na chama hicho, baada ya kujitoa CCM.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa leo amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Lowassa amechukua fomu hio Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mamia ya wanachama wa Chadema na viongozi wa juu wa Chama hicho.

No comments: