Baadhi
ya wateja wakiwa ndani ya Airtel smartphone Bazaar ili ku smartiphonica na simu
za kisasa kwa bei poa.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza offa kabambe ya simu za kisasa
itakayopatikana katika viwanja vya nane nane kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 31
julai 2015, kwa muda wa siku 10 Akiongea kuhusu ofa hiyo Meneja Masoko wa
Airtel Bi Aneth Muga amesema, Airtel inaendelea kuwapati wateja wake
mawasiliano bora na kuwaunganisha na simu za kisasa zilizounganishwa na
vifurushi vya bure vya internet katika msimu huu wa nanenane".
"Napenda
kuwajulisha watanzania wote na wakazi wa Morogoro kuwa Airtel sasa
tumewafikia na kusogeza huduma zetu karibu nao katika viwanja vya nanenane
ambapo tutakuwa na offa nyingi ikiwemo simu za kisasa ya aina ya Airtel Led
itakayounganishwa na huduma za internet bure kwa mwaka mzima kwa gharama ya
shilingi 75,000.
Sambamba
na Airtel Red pia tunazo simu za aina nyingi ambazo ni pamoja na simu ya
Huawei , Techno, Samsaung. Simu hizi zinamuwezesha mteja kuzitumia katika
kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutunza rekodi zao, inatumika kama kamera
ya kupiga picha pamoja na mambo mengine mengi. Tunatoa
wito kwa wateja wetu watembelee banda la Airtel katika viwanja ya
Nanenane na kupata nafasi ya kununua simu hizi za kijanja kwa gharama nafuu "aliongeza
Muga.
Airtel
Smartphone Bazaar bado pia iko jijini Dar es Salaam katika maduka yote ya
Airtel. Khalikadhalika wateja wote bado pia wananafasi ya kusmatiphonica kwa
kutembelea maduka ya Airtel nchi nzima.
No comments:
Post a Comment