Tangazo

August 26, 2015

FIRST NATIONAL BANK (FNB) YAFUNGUA TAWI MBEZI BEACH JIJINI DAR

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam huku akiambatana na Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo na Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha.
Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Mitandao, Silvest Arumasi akimpa maelekezo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mara baada ya kufungua rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo.
Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha akiongea machache wakati wa ufunguzi rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa benki ya First National kwa kuendelea kufungua matawi yake pembezoni mwa mji wa Dar es Salaam ambapo alisema ni jambo la faraja sana pale mteja anapofuatwa alipo na si kila siku kukimbilia kufungua benki katikati ya mji. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili toka kulia) akiwa na Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo ( kwanza kulia) pamoja na viongozi wa benki ya First National. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja, Francois Botha na Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Mitandao, Silvest Arumasi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea machache na mmoja ya kiongozi wa Benki hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya First National na wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda  akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari. 

Ikiwa ni sehemu ya mkakati wake kuwafikishia Watanzania wengi zaidi huduma za kibenki na kukuza uchumi, First National Bank imefungua tawi Mbezi Beach na kufanya idadi ya mtandao wa matawi yake kufikia nane. 

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo jipya lililopo Shamo Towers Mbezi, mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja wa benki hiyo Francois Botha amesema leo kwamba ufunguzi wa tawi hilo ni sehemu ya mkakati wa kufikisha huduma za kibenki katika maeneo yote muhimu ya jiji la Dar es salaam na nchi nzima na kuinua uchumi wa Watanzania kupitia huduma mbalimbali kama mikopo ya nyumba na mikopo kwa wafanyabiashara wadogo,wa kati na wakubwa. 

 “Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishii Mbezi na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa kasi,” alisema Botha. 

 Mkuu wa kitengo cha bidhaa na huduma za kidigitali wa First National Bank, Silvest Arumasi, alisema kuwa kutokana na ukuaji wa kasi wa jiji la Dar es salaam benki hiyo imeona umuhimu wa kuhakikisha huduma za kisasa za kibenki zinawafikia watu wengi zaidi.  

“Tunataka kuhakikisha tunatoa mchango muhimu katika kuendeleza sekta ya fedha nchini na tumepanga kuendelea kuanzisha huduma mpya zenye ubunifu na za kitaalamu hapa nchini,” alisema Arumasi. Tawi hilo lililofunguliwa Mbezi Beach Shamo Towers litatoa huduma za kibenki mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo.

No comments: