Tangazo

September 10, 2015

LOWASSA, DUNI WAHUDHULIA UFUNGUZI WA KAMPENI ZA CHAMA ZA CUF, ZANZIBAR

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, Nassor Mazrui, wakati akiwasili katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI, ZANZIBAR
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akilakiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA-Zanzibar, Salum Mwalim, wakati akiwasili katika Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Juma Duni Haji, akiwapungia wananchi wa Zanzibar (hawapo pichani) walioshiriki Ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, katika hafla ya Ufunguzi wa Kampeni za Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Mgombea Urais wa Ukawa wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za CUF, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.
Wakubwa wakiteta jambo.
Wimbo maalum wa Chama cha Wananchi CUF ukipigwa.
Maalim Seif akiongoza ufunguzi wa Kampeni hizo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia kwenye Mkutano huo.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Juma Duni Haji, akiwasalimia wazanzibar.




No comments: