Tangazo

October 22, 2015

Airtel Smartifonika yaleta simu mpya sokoni nafuu kuliko zote

Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki (kushoto) na  Meneja masoko wa Airtel Anethy Muga (kulia) wakionyesha simu mpya zilizoingizwa sokoni zikiwa na ofa ya Airtel smartifonika aina ya Mgnum Bravo Z10 wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Airtel leo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Octoba 22, 2015 
Airtel Tanzania leo imezindua smartifoni mpya na yenye ubora zaidi ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 ambapo zinapatikata sasa hivi  kwenye maduka yote ya Airtel nchini zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  inayompatia mteja muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga amesema “Airtel tumekuletea Simu mpya ya Magnus Bravo Z10 ili kukuwezesha mteja wetu kuendelea kufurahia huduma zote za Airtel na zile huduma zote za kisasa za smartifoni ukiwa mahali popote
 “Magnus Bravo Z10 toka Airtel inatumia laini mbili, ina radio, kioo (screen) kubwa ili kukupa raha zaidi kuona vyema unapokuwa unaitumia, pia imewekewa kamera zenye uwezo mkubwa mbele na nyuma za 5mp ili kukupa taswira au picha nzuri utakazopiga karibu au mbali ukiwa na ndugu, jamaa na marafiki” alielezea Bi Muga
“Vilevile ili  uweze kufurahia huduma zote za mitandao, Airtel tumehakikisha tayari simu hii inamitandao yote ya kijamii kama facebook, Instagram, twitter na mingine mengi” . Alisema Bi Muga

Simu hii inapatikana sasa katika maduka yote ya Airtel nchini kwa gharama nafuu kuliko zote ya sh. 75,000  tu.

No comments: