Tangazo

October 1, 2015

Airtel yatoa gawio la Shilingi Bilioni 5.3 kwa wateja wa Airtel Money

Meneja biashara wa kitengo cha  Airtel Money,  Bw. Asupya Naligingwa(kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza Airtel kugawa gawio la faida la zaidi ya  shilingi billion 5 kwa wateja na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima. Kushoto  ni Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bi. Jane Matinde.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Dar es Salaam

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kugawa zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa wateja na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima.

Uamuzi huo wa kutoa gawio la faida lililopo katika akaunti  ya udhamini ya wateja wa Airtel Money (Trust account)  litawawezesha wateja wa Airtel kulipwa kiwango kizuri cha gawio la faida.  Kiwango hiki cha pesa kitalipwa kutokana na  kiasi cha pesa mteja alichokuwa nacho kwenye akaunti yake ya Airtel Money kila mwisho wa siku  kuanzia March 2014 hadi April 2015.

Akiongea na waandishi wa habari,Meneja wa kitengo cha  Airtel Money, Asupya Nalingigwa, alisema wanayo furaha kutangaza mgawanyo  huu wa gawio la faida kwa wateja wao baada ya benki kuu ya Tanzania. Kuidhinisha kutoa  pesa hizi katika akaunti ya udhamini ya pesa za
wateja wa Airtel Money ijulikanayo kama trust  account.

Aliongeza kwa kusema wateja wa Airtel Money watapata sehemu ya gawio lao  kulingana na salio wanalokuwa nalo kwenye akaunti zao kila siku.


"Tunaamini kiasi hiki cha pesa kitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha maisha ya watanzania wengi , kuwahamasisha wateja wasiofikiwa na huduma za kibenki kutumia mfumowa pesa kwa njia ya simu. Vilevile wateja wetu wa Airtel Money wataendelea kutumia huduma za pesa kupitia simu za mkononi, kufanya miamala yao ya kila siku na kutunza pesa zao ili kupata gawio lao kila watakapo weka pesa katika akaunti zao za Airtel Money". Aliongeza Nalingigwa

Uamuzi huu wa kutoa gawio la faida kwa wateja ni wakuungwa mkono kwani unachochea na kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi , ukizingatia takribani asilimia 85% ya watanzania bado hawajafikia na huduma za kibenki.

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za kibunifu  za kifedha kupitia simu za mkononi ikwemo NFC huduma inayokuwezesha kufanya malipo kupitia kadi, Mikopo ya Timiza na huduma nyingine nyingi.

Katika  maelezo yake Naligingwa aliahidi  Airtel kuendelea na dhamira yake ya kuzindua huduma bora na za kisasa katika mienzi ijayo ili kuwanufaisha watanzania waishio maeneo ya mijini na vijijini


About Bharti Airtel
Bharti Airtel Limited is a leading global telecommunications company with operations in 20 countries across Asia and Africa. Headquartered in New Delhi, India, the company ranks amongst the top 3 mobile service providers globally in terms of subscribers. In India, the company's product offerings include 2G, 3G and 4G wireless services, mobile commerce, fixed line services, high speed DSL broadband, IPTV, DTH, enterprise services including national & international long distance services to carriers. In the rest of the geographies, it offers 2G, 3G and 4G wireless services and mobile commerce. Bharti Airtel had over 335 million customers across its operations at the end of August 2015. To know more please visit, www.airtel.com<http://www.airtel.com>

No comments: