Tangazo

October 5, 2015

OMARY KIMBAU "Jembe": Jimbo la Mafia 2015 ni la UKAWA kwa maendeleo ya Wanamafia

    DSC_2369.jpgssssssssssssssss DSC_2368
Moja ya Bango kubwa la "JEMBE" la Mgombea Ubunge wa jimbo la Mafia kwa tiketi ya UKAWA, Ndugu Omary Kimbau maalufu kama JEMBE akiwa pamoja na Madiwani wake katika Kata nane za Jimbo hilo la Mafia katika Wilaya ya Mafia ndani ya Kisiwa cha Mafia.Na 

Mwandishi Wetu,

[MAFIA-PWANI] Wananchi wa jimbo la Mafia, jimbo lililopo katika Wilaya ya Mafia ndani ya kisiwa hicho cha Mafia, Mkoa wa Pwani chenye jumla ya Kata Nane, wameombwa kujitokeza kwa wingi Oktoba 25, mwaka huu wampigie kura kwa wingi mgombea wa UKAWA, Omary Ayub Kimbau maalufu kama “JEMBE” ili akawawakilishe Bungeni pamoja na kuwapigania katika kudai haki zao wanamafia.

Hayo yameelezwa kisiwani hapa katika kampeni za mgombea huyo wa Ubunge wa UKAWA, kutokea chama cha Wananchi CUF.

Omary Kimbau ambaye kitaaluma ni msomi wa Biashara na Mwana-Dipromasia, ameweza kufunguka kuwa yeye ni miongoni mwa wanasisa vijana walioweza kupikika kisiasa na kisomi hivyo lengo kuu la kuweza kuwakomboa wananchi wa jimbo hilo ni kumpa nafasi ya kumchagua ili kwenda kuwatetea wananchi wa jimbo hilo pasipokuangalia mtu huyo ametokea familia ya nani ama chama gani kikubwa ni kuakikisha wanampigia kura za wingi za ushindi yeye pamoja na madiwani wote kupitia UKAWA.

“Mimi ni mfanyabiashara na Mwanadipromasia niliyesomea kitaaluma. Nitaendelea kufanya siasa na kusimamia haki kwa wananchi wa jimbo la Mafia na wala si matusi kama wanavyotufanyia wapinzani wetu upande wa pili. Nawaombeni wananchi Oktoba 25, tujitokeze kwa wingi na kukipigia kura CUF kupitia mimi mgobea wenu.. OMARY KIMBAU… pamoja na madiwani wangu wote” alieleza Kimbau katika mkutano huo wa kampeni huku akishangiliwa na umati wa watu wa kijiji hicho cha Banja.

Pia alifunguka kuwa, yeye ndio alikuwa diwani mdogo kuliko wote Tanzania na Duniani aliyewahi kutokea katika ulimwengu wa kisiasa, kwani mwaka 2005, aliweza kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Kijitonyama ambapo alikaa kwa kipindi kimoja hadi 2010, ambapo aliacha nafasi hiyo na kwenda kugombea Ubunge ndani ya CCM hata hivyo alinyimwa haki hiyo kwa kuelezwa kuwa yeye ni mdogo licha ya kushinda katika kura za maoni ndani ya chama hicho.

Na kuendelea kusema kuwa, mwaka huu 2015, aligombea tena ndani ya chama cha CCM, katika kura za maoni alifanyiwa zengwe hivyo kukihama chama hicho na kujiunga na CUF ambapo anagombea kwa sasa ndani ya jimbo hilo ambalo amelielezea kuwa anatosha kuvaa viatu vyake.

Hata hivyo aliwataka wanamafia kuachana na kuwapuuza wapinzani wanayoeneza juu ya kumuhusisha na baba yake aliyewahi kuwa kada wa chama hicho cha CCM na mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20, na kusema kuwa: “CCM wanatapatapa.. na hawana pa kutokea, Hili jimbo ni la “Jembe”. Kule Marekani kulikuwa na Rais George W. Bush ambaye baba aliwahi pia kuliongoza taifa hilo.. tena taifa kubwa Bush alitokea upinzani na wakampa wanachoangalia ni sera na utawafanyia nini.

Kwa hapa hapa Tanzania tu Amani Karume, aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kati ya mwaka 2000 hadi 2010, ni mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume mbona hawasemi hilo.. kule Kenya sasa inaongozwa na Uhuru Kenyatta ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Taifa hilo, Jomo Kenyatta.

Kule Msoga mbunge katika jimbo la Chalinze ni Ridhiwan Kikwete ambaye amechukua nafasi hiyo kwa sasa jimbo hilo liliwahi kutawaliwa na baba yake mzazi ambaye sasa ni Rais, Jakaya Kikwete mbona hilo hawalisemi ama ndio kunya anye kuku na akinya bata mchafu” alihoji Kimbau huku akishangiliwa na watu ambapo pia aliwataka kuwapuuza watu hao kwani hawana nia njema na jimbo hilo kwani mgombea huyo anatumia wadhifa wa kaka yake anyemwendesha kama ‘rimoti’

Katika hali ya kushangaza wakati wa mkutano huo ukiendelea majira ya saa 10 jioni, ilitokea vulugu zilizosababishwa na chama cha Mapinduzi CCM baada ya mgonbea wake kufika jirani na mkutano huo wa CUF na kisha kufanya mkutano wake ambao haukuwa kwenye ratiba.

 Kufuatia hali hiyo, Wanachama wa CUF waliokuwa kwenye mkutano huo wa JEMBE, waliweza kukimbilia wote na kuvamia mkutano wa CCM wakitaka kujua kulikoni, lakini mgombea wa CCM, Mbaraka Dau aliweza kuokolewa na kukimbizwa kufichwa kwenye nyumba ya jirani kabla ya kutolewa kupitia kichakani na kutokomea kusiko julikana.

Vurugu hiyo iliyodumu kwa muda wa zaidi ya dakika 40, ziliweza kuamsha hasira za wana UKAWA na wanachi wa Kijiji hicho waliojitokeza kwa wingi walilalamikia hatua ya CCM kuingilia mkutano ya wapinzani kwani wanaweza kusababisha vitendo vya uvunjifu wa amani.

Hata hivyo baada ya vamizi hilo wanachama wa CUF waliweza kuwaambia wanachama wa CCM walioachwa na Mgombea wa CCM, Mbaraka Dau kuwa, wao hawatafanya fujo, ila walimtaka aondoe gari yake na asionekane hapo kwani wangemkamata mgombea huyo wangemfungulia mashitaka na hata kufungwa kwa uchochezi.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hzi alipomtafuta mgombea huyo hakuweza kupokea simu yake ambayo muda wote ilikuwa ikiita bila majibu lakini alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi juu ya tukio hilo la kutaka kuvuruga amani dhidi ya mkutano halali wa CUF, aliweza kujibu ujumbe huo kwa kueleza kukana kuwa si kweli.

Katika kampeni hizo imeelezwa kuwa, mgombea huyo wa CCM amekuwa akipita na kugawa rushwa ikiwemo kuwapa wananchi pesa bandia huku wengine wakishikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na pesa bandia kwani licha ya kueleza wamepewa na mbunge huyo lakini jeshi ihilo limeshindwa kumchukukia hatua zozote.

“Si mara ya kwanza hii. Wamekuwa wakitufuatilia kila tunapofanya mkutano wetu, nao wanaweka mkutano wao hatua chache kutoka tulipo sie” alieleza Kaimu Mwenyekiti wa CUF Wilaya hiyo, Faki Ally.

Kwa upaande wake mjumbe wa Mkutano mkuu wa CUF, Amdan Rashid Mwichande alieleza kuwa, fujo hizo wanazofayiwa ni hira mbaya za CCM baada ya kuona wamebana kila idara, ambapo amebainisha kuwa vitendo vitakuja kuwahukumu na wao wataendelea kufanya kampeni za kistaharabu wala hawatafanya fujo wala matusi ilikujiakikishia ushindi wa kishindo.

“Sie tunanadi sera zetu pekee. Kama wamezoea kuona wapinzai wanatoa matusi basi wasahaau kwa hilo. Sie tunaendeleza sera zetu ikiwemo suala la Afya, Elimu, Miundombinu, suala la hifadhi ya bahari ambalo linawanyima wanamafia wengi fursa ya kutumia bahari yao waliopewa na Mungu na suala la usafiri wa uhakika wa Mfia” alieleza Mwinchande.

Mkutano huo uliofanyika juzi jioni ulikuwa ni mkutano wa saba kwa mgombea huyo wa UKAWA ambaye anatarajia kuendelea tena na kampeni zake kesho huku mikutano mingine ya Kila Kata na kijiji ikiendelea kila siku.
DSC_2067
Wafiasi wa UKAWA wakimpokea Mgombea ubunge wa jimbo Omary Kimbau 'Jembe' wakati alipowasili katika uwanja wa kampeni.
DSC_2076
Omary Kimbau akiwasilia kwenye mkutano huo..
DSC_2070
DSC_2080
DSC_2082
Mgombea Ubunge wa kupitia UKAW, jimbo la Mafia, Omary Kimbau (kulia) akipokelewa na Kada wa CUF katika kijiji hicho cha Banja.
DSC_2166
DSC_2168
DSC_2201
DSC_2165
Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Mafia wa CUF, Faki Ally..
DSC_2205
DSC_2207
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kirongwe kwa tiketi ya UKAWA, chama cha CUF, Mohamed Tukhi (kushoto) akifuatilia mkutano huo anayefuatia ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Amdan Rashid Mwinchande.
DSC_2237
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Amdan Rashid Mwinchande akitoa sera wakati wa mkutano huo wa kumnadi mgombea wa Ubunge wa UKAWA, Omary Kimbau JEMBE, katika mkutano huo uiofanyika kijiji cha Banja Kata ya Kirongwe.
DSC_2249
Amdan Rashid Mwinchande akipeana mkono na Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo Omaary Kimbau JEMBE..
DSC_2234
Wanachama wa CUF wakiserebuka wakati wa mkutano huo..
DSC_2262
Faki Ally akimnadi mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kirongwe, Mohamed Tukhi..
DSC_2266
DSC_2267
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mafia kwa tiketi ya UKAWA, Omary Kimbau JEMBE , akisalimiana na mgombea Udiwani wa Kata ya Kirongwe, Mohamed Tukhi mara baada ya kumaliza kunadi sera katika Kata hiyo...
DSC_2281
Mgombea Ubunge wa jimbo laa Mafia kwa tiketi ya UKAWA, Omary Kimbau akinadiwa na Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Faki Ally..
DSC_2288
DSC_2292
DSC_2303
Omary Kimbau JEMBE wa UKAWA/CUF anayegombea Jimbo hilo akijinadi katika mkutano huo wa kampeni katika Kata ya Kirongwe kwenye kijiji cha Banja..
DSC_2312
Baadhi ya wananchi wakimsikilia Mgombe wa Ubunge kupitia chama cha wananchi CUF na UKAWA, Omary Kimbau JEMBE, katika mkutano huo wa kampeni katika kijiji cha Banja, Kirongwe.
DSC_2214
Baadhi wananchi na wafuasi wa UKAWA wakifuatilia mkutano huo.. wakati Omary Kimbau JEMBE akihutubia jukwaani (Hayupo pichani).
DSC_2316
Omary Kimbau JEMBE anayegombea jimbo hilo akitoa fursa za kuulizwa maswali na wananchi wowote wale wa kijiji hicho cha Banja na kujibu ambayo aliielezea ni njia ya demokrasia katika siasa za kisomi na maendeleo..
DSC_2328
Omary Kimbau JEMBE anayegombea jimbo hilo la Mafia akiwanadi wagombea wa Udiwani wa Kata nane za jimbo hilo..
DSC_2359
Wananchi katika mkutano huo..
DSC_2332
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kilindoni, Mbonde Mussa akijieleza katika mkutano huo wa kampeni wa kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Omary Kimbau..
DSC_2339
Mgombea Ubunge wa Kata ya Kiegani, Seleman Darushi akijinadi katika mkutano huo..
DSC_2350
Mgombea udiwani wa Kata ya Baleni, Omary Baruti akiomba kura..
DSC_2380
Kikundi cha hamasa katika mkutno huo cha Rambaramba,wakionesha umahiri wao wa kuimba mashahiri ya papo kwa hapo yanayoendana na kero na matatizo ya jimbo hilo..
DSC_2397
Amdan Rashid Mwinchande akiwa katika picha ya pamoja na Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo Omaary Kimbau JEMBE na vijana wa hamasa wa chana hicho
DSC_2125
Baadhi ya wanachama wa UKAWA wakiwa wamejawa na hasira baada ya kuvamiwa katika mkutano wao huo na wanachama wa CCM wakiongozwa na mgombea ubunge wao Mbaraka Dau...
DSC_2141
Gari la Mgombea Ubunge wa CCM, Dau likiwa limezingira baada ya mgombea huyo kukimbia na kufichwa chooni kwa kuogopa kipigo kutoka kwa wananchi na wanachama wa UKAWA wenye hasira ambao walimtaka aondoke kwani hakuwa na ratiba ya kufanya mkutano katika Kata hiyo...
DSC_2146
..Gari hilo la Mgombea la CCM likiondoka katika eneo la jirani na ulipokuwa mkutano wa mgombea ubunge wa UKAWA, Omary Kimbau JEMBE.. Gari hilo liliondoka mahala hapo baada ya wanachama na wananchi kupiga kelele kutaka liondoke na mgombea wao kutoonekana kabisa hapo kwani haukuwa mkutano wao hivyo endapo lingekuwa hapo wangelichoma moto..
DSC_2149
Wananchi na wanachama wa UKAWA pamoja askari wakishuhudia gari hilo likiondoka katika eneo hilo ili Mgombea wa UKAWA aendlee na mkutano wake halali uliokuwa kwenye ratiba..
DSC_2177
Umati mkubwa wa nanchi wa Kijiji cha Banja wakirudi kwa shangwe na furaha baada ya kufanikiwa kumuondoa mgombea Ubunge kupitia CCM, aliyekuwa amefika hatua chache kwenye mkutano wa UKAWA na kuanza kampeni yake.. kundi hilo liliweza kurudi kwenye eneo hilo huku wakishangilia kwa ushindi huo kwa kuzishinda hila za CCM ambazo walidai kuwa wamekuwa wakifanya hivyo kila mikutano ya UKAWA inapofanyika.
DSC_2097
DSC_2099
wananchi katika mkutano huo...
kk;a
..Mgombea Ubunge wa UKAWA, Omary Kimbau JEMBE akiwa na mgombea Udiwani wa Kata ya Kilindoni, Mbonde wakiwa katika maandalii wakati wa kuelekea kwenye kampeni ambapo waliweza kujumuika pamoja na wananchi kwa lengo la kupata chakula.
DSC_2062
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mafia kwa tiketi ya UKAWA, Omary Kimbau JEMBE akibadilishana mawazo na wananchi kwenye jiwe cha kahawa na bao katika eneo la Kigamboni ndani ya Kilindoni, Mafia.

No comments: