Tangazo

November 17, 2015

Kampuni ya LETSHEGO/Faidika yapata asilimia 75 ya hisa katika benki ya Advans Tanzania!

DSC_1794
Mtendaji Mkuu wa Afrika Mashariki wa kampuni ya Letshego, Bwana Tom Kocsis akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho mpya wa kununua hisa asilimia 75 za benki ya Advans Tanzania. wengine ni maafisa waandamizi wa kampuni hiyo (Picha zote na Andrew Chale)

Na Andrew Chale, Modewjiblog

[DAR ES SALAAM-TANZANIA] Kampuni ya LETSHEGO Holding Limited yenye makao yake makuu nchini Botswana ambayo kwa Tanzania ikijulikana kama taasisi ya Mikopo ya Faidika, imetangaz kupata asilimia 75 ya hisa kutoka katika benki ya Advans ya Tanzania kwa kununua hisa moya kwa shilingi Bilioni 15.5 ambazo ni sawa na dola za Kimarekani Milioni 7.

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es Salaam, viongozi wakuu wa Faidika na Advans Tanzania wamebainisha kuwa sasa huduma za kifedha nchini zimeongezeka maradufu hivyo ni fursa za kipekee kwa watanzania wakiwemo wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma katika benki hiyo ya Advans.

"Kufanikiwa kwa Faidika, kunaongeza uwekaji wa akiba, malipo, mikopo ya biashara ambayo ni moja ya mikakati yetu kwa wateja wetu. Hii pia itaruhusu benki ya Advans kutoa mchango mkubwa kwa Serikali ya Tanzania" ameeleza Mkurugenzi Mkuu wa Letshego Group, Chris Low katika tukio hilo.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa, Benki kuu ya Tanzania (BOT) imeipatia kibali taasisi hiyo ya Faidika kuwa wakala wa benki ya Advans wa kutoa huduma za kibenki kwa niaba ya benki hiyo, katika vituo takribani 105.

Hata hivyo Letshego inaamini kuwa mafanikio hayo ni ishara tosha ya kutoa huduma bora kwa watu wote ikiwemo wale wa kipato cha chini, kati katika jamii ambao kihistoria hawajaweza kupata huduma stahiki katika benki za biashara hivyo mfumo mzuri wa kuwezesha jamii kupata huduma za kifedha, Letshego imekuja wakati muafaka wa kusaidia Serikali kuinua uchumi.

Letshego/Faidika kwa Tanzania inatoa huduma zaidi ya Watanzania 44,000 kupitia taasisi yake hiyo ya mikopo ya Faidika huku bidhaa na huduma zake pia zikipatikana kupitia mitandao wenye matawi zaidi ya 105 na ofisi za Satelaiti huku ikiwa na timu ya maafisa mauzo wapatao 230.
DSC_1778
Mkurugenzi Mtendaji wa Advans Tanzania, Bwana Tanguy Gravot (wa kwanza kulia) akizungumza kwenye mkutano mkutano huo. Wengine ni maafisa kutoka kampuni ya Letshego ambao wamenunua hisa asilimia 75 kwa benki hiyo ya Advans Tanzania.

Kwa upande wao benki ya Advans Tanzania wamepongeza kampuni ya Letshego kuwa mbia mkuu wa benki hiyo kwa njia ya uuzwaji wa hisa. Kwa hatua hiyo Letshego atakuwa mwanahisa mkuu huku wale wanahisa waanzilishi wa benki hiyo wakiwemo Advans SA na FMO watabaki kuwa wanahisa wadogo wa kampuni.

"Umoja ulioundwa kati ya kampuni hizi mbili utaiwezesha benki ya Advans Tanzania kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wote wakiwemo wale wadogo, wa kati na wakubwa kwa maeneo yote huku pia kuongeza wigo wa kijiografia za huduma." alieleza Mkurugenzi Mtendaji wa Advans SA, Bw. Claude Falgon.

Kwa hatua hiyo, Advans inaamini kuwa wajasiriamali waadogo na wa kati ni wakati wa kuchangamkia fursa zaidi katika benki hiyo.

Advans ya Afrika Kusini (Advans SA) ni kampuni iliyoundwa tokea mwaka 2005 na Developement Finance 9Horus) pamoja na Eid,KfW, FMO, CDC Group plc, AFD group na IFC huku shughuli yake kubwa ikiwa ni kutengeneza mtandao wa taasisi ndogo ndogo za kifedha (MFIs) katika nchi zinazoendelea na zinazoinukia ilikutoa huduma za kifedha kwa wajasiliamali wadogo na wa kati.

Mtandao wa Advans umesambaa karibu dunia nzima ambapo pia waweza kutembelea mtandao wa : www.advansgroup.com
DSC_1807
Mkurugenzi Mkuu wa Letshego Group, Chris Low (katikati) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa shughuli hiyo ya kutangaza kuingia ubia na benki ya Advans Tanzania.
DSC_1801
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia shughuli hiyo..
DSC_1826
Mmoja wa wajumbe wa Bodi wa Taasisi ya mikopo nchini ya Faidika, Dk.Ellen Otaru Okoedion akielezea fursa za mikopo inayotolewa na Faidika huku akitumia wasaha huo kuwaomba wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma za kibenki na mikopo zinazotolewa na Faidika pamoja na benki ya Advans Tanzania.

No comments: