Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil
Colaso akionyesha tuzo mbili za ubora mara baada ya kukabidhiwa na waandaji wa
Tanzania Leadership Award 2015. Airtel ilijishindia tuzo hizo katika kipengele
cha kutoa huuduma za kimtandao pamoja na huduma zinazokidhi mahitaji ya wateja katika
sekta ya mawasiliano.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
* Yajishindia tuzo kwa
matumizi bora katika kutoa huuduma za kimtandao pamoja na huduma zinazokidhi mahitaji
ya wateja
Dar es Salaam,
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma za kibunifu imetunikiwa tuzo mbili za
ubora za Tanzania Leadership Awards 2015 katika halfa iliyofanyika katika
hotel ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
Airtel imejishindia tuzo hizo katika kipengele
cha matumizi bora ya huduma za kimtandao kufikia wateja wake (best use of
social Media in marketing) pamoja na kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya
wateja (brand excellence) katika sekta ya mawasiliano na kuwashinda makapuni mengine
yaliyokuwa wakichauana nayo katika kinyanganyiro cha tuzo hizo.
Wakiongeza wakati wa kukabidhi tuzo
hizo , waandaaji wa tuzo hizo za Tanzania Leadership awards, Bwana Kishore
Bollakpalli alisema " Airtel imepata tuzo hizi kutokana na kufanya vizuri
zaidi katika kuwasiliana na wateja wake kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii
na hivyo kuwafikia wateja wake nchini nzima kwa urahisi zaidi. Lakini kwa upande
wa tuzo ya Brand excellence, Airtel imeonyesha kwa vitendo dhamira yao ya kutoa
huduma bora kwa wateja wake huku ikitoa bidhaa na huduma za kibunifu ili
kukidhi mahitaji ya wateja wake na kuboresha maisha yao.
Akipokea tuzo hizo Mkurugenzi Mkuu wa Airtel,
Bwana Sunil Colaso alisema" Tunayofuraha kupokea tuzo hizi za Tanzania
Leadership award na tunaamini huu ni ushuhuda kamili unaoonyesha kwa
vitendo dhamira yetu ya kutoa huduma zenye zinazokidhi mahitaji ya wateja
wetu zikiwemo huduma za intaneti, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na
kuchochea kukua na upatikanaji wa huduma za kifedha nchini".
Colaso aliongeza kwa kusema Airtel itaendelea na dhamira yake yakutoa huduma zinazogusa mahitaji ya wateja wake u na kuwaweka karibu ili kuendelea kutoa huduma bora zaidi katika miaka ijayo.
Tuzo za Tanzania Leadership Awards zinalenga kutambua na kupongeza jitihada zinazofanya na watu binafsi na makapuni katika kuboresha uchumi wa Tanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment