Tangazo

December 10, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA MAADHIMISHO YA NANE YA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI, JIJINI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipunga mkono kupokea maandamano ya wananchi kwenye Viwanja vya Karimjee katika Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Dec 10, 2015. Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Bahame Nyanduga, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kupokea maandamano ya wananchi wakati wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, wakati wa mapokezi ya maandamano ya wananchi wakati wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Maimuna Tarishi, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Makamu wa Rais kuhutubia wakati wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Ofisi ya Tanzania, Joyce Mends-Cole, akizungumza kabla ya Mhe. Makamu wa Rais kuhutubia wakati wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wananchi na wadau mbalimbali waliohudhuria ufunguzi huo wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na mtoto, Ahana Gloria Massey (5) wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Dec 10, 2015 katika ufunguzi wa maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na washiriki wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Nane ya Kitaifa ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, baada ya ufunguzi huouliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.

No comments: